******************************
TAREHE 12.04.2020 MAJIRA YA 20:05 HRS USIKU HUKO
KATIKA BARABARA YA MAKONGORO, ENEO LA KIFUA
WAZI – ROCKY MALL, KATA YA KIRUMBA, WILAYA YA
ILEMELA, MKOA WA MWANZA, GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T.263 CZQ TOYOTA HAICE – DALADALA
LINALOFANYA SAFARI ZAKE ZA KISESA – NYASAKA
MZUNGUKO, LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA EMMANUEL S/O MWANASALAHA,
ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 25
HADI 30, LIKITOKEA MJINI KWENDA NYASAKA. GARI HILO
LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEKUWA AKIVUKA
BARABARA TOKA UPANDE MMOJA KWENDA UPANDE WA
PILI AITWAYE JOSEPHAT TONER, MIAKA 40, MSUKUMA,
MKAZI WA GHANA –MWANZA, (MWENYE ALBINISM) NA
MKURUGENZI WA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI (NGO)
LIJULIKANALO “TONER FOUNDATION” NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE.
BAADA YA TUKIO HILO DEREVA ALITELEKEZA GARI NA
KUKIMBIA, JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA
KUSHIRIKIANA NA MMILIKI WA GARI HILO NA WANANCHI
KWA UJUMLA WANAMTAFUTA DEREVA ALIYEKIMBIA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE
KUCHUKULIWA.
UCHUNGUZI KUHUSU AJALI HII UNAKAMILISHWA. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA
MKOA – SEKOU TOURE KUSUBIRI UCHUNGUZI WA DAKTARI.
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MWILI UTAKABIDHIWA
KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUTOA WITO KWA
MADEREVA WOTE WA VYOMBO VYA MOTO NA WATEMBEA
KWA MIGUU KUENDELEA KUWA MAKINI NA KUFUATA
SHERIA WAKATI WANAPOTUMIA BARABARA.