**************************
KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia Pamoja na vifaa vya kutengenezea noti hizo.
Ni kwamba mnamo tarehe 11.04.2020 majira ya saa 00:30 usiku huko eneo la Sokoni, Kata ya Kyela Kati, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.
Jeshi la Polisi mkoani hapa lilimkamata JOHN FRANCIS [22] mfanyabiashara na mkazi wa Olofea – Kyela akiwa na noti bandia dola za kimarekani 09 kila noti sawa na dola 100 kama zingekuwa halali sawa na dola 900 zikiwa na Na. LB399120505B, noti za Zambia Kwacha 40 kila noti sawa na noti za Zambia kwacha 100 kama zingekuwa halali sawa na kwacha 4,000. kati ya noti 20 zina Na. EH122082777 na noti nyingine 20 zina Na. EH122082854.
Wakati huo huo katika misako inayoendelea katika maeneo mbalimbali, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya lilimkamata PETER MWAKAMENYA [37] Mkazi wa Mbalizi akiwa na noti bandia 07, noti 02 Tshs.10,000/= Na.HJ5091884 na
Tshs.5,000/= Na.EY2592056, noti 02 dola za Kimarekani 200 Na.LB39120505BBZ kama zingekuwa halali sawa na dola 200, noti 03 za Zambia Kwacha Na.EH122082777, EH12208254, EH122082777 kila moja sawa na Kwacha 100 kama zingekuwa halali sawa na Kwacha 300. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Mnamo tarehe 10.04.2020 majira ya saa 11:00 Asubuhi huko Mtaa wa Relini, Kitongoji na Kata ya Bwawani, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ZEZE CHARLES [29] mkazi wa Bwawani akiwa na Pikipiki Na. MC 417 CAR Sinorai, Chasis Na. LD3PCK6J5J2004712 mali ya wizi. Thamani ya Pikipiki ni Tshs. 2,200,000/=. Upelelezi unaendelea.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 10.04.2020 majira ya saa 15:30 Alasiri huko maeneo ya sheli ya Tanganyika iliyopo Mtaa wa Sokoni, Kata ya Makongolosi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi waliwakamata KULWA
WATSON [42] na STEWARD CHARLES [25] mchimbaji madini wote wakazi wa Makongolosi wakiwa na bhangi kilogramu 03. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa bhangi.