Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, Kanda ya Ziwa, Sibtain Meghjee (kulia) akifurahia jambo wakati Sheikhe Hasani Kabeke, ambaye ni Sheikhe wa CCM Mkoa wa Mwanza akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa vitakasa mikono 7 vilivyotolewa jana na taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania .Picha na Baltazar Mashaka
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikhe Hasani Kabeke (kulia) akiwaongoza kusoma dua baadhi ya masheikhe na waumini wa misikiti iliyonufaika na msaada wa manteki ya maji na sabuni kwa ajili ya kutakasa mikono katika mapambano ya virusi vya corona.
Katika vita ya kupambana na virusi vya Corona, Mwenyekiti wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya ya Ziwa, Sibtain Meghjee (kushoto) jana, akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikhe Hasani Kabeke matenki ya maji saba pamoja na sabuni kwa ajili ya kutumiwa na waumini wa Kiislamu kutasa mikono katika misikiti ya BAKWATA mkoani humu.Msaada huo umegharimu sh. milioni 1.5.Picha na Baltazar Mashaka.
Sheikhe wa CCM Mkoa wa Mwanza, Sheikhe Hasani Kabeke akinawa mikono baada ya kupokea msaada wa matenki saba ya maji na sabuni, uliotolewa na taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya Ziwa huku Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain Meghjee akishuhudia.Picha na Baltazar Mashaka.