***************************
TUKIO LA KWANZA
TAREHE 10.04.20202 MAJIRA YA 04:00HRS ALFAJIRI, HUKO KIJIJI CHA NYAMANGA, KATA YA UKARA, WILAYANI
UKEREWE, PASTORY MAJURA, MIAKA 52, MSUKUMA,
MKAZI WA KIJIJI CHA NYAMANGA – UKEREWE, ANATUHUMIWA NA KOSA LA MAUAJI BAADA YA KUMUUA
MKEWE AITWAYE ANUSIATA JAMES, MIAKA 52, MZINZA,
MKAZI WA KIJIJI CHA NYAMANGA, KWA KUMPIGA
KICHWANI NA KITU KIZITO BAADA YA KUMFUMANIA MKE
WAKE NYUMBANI KWAKE AKIWA NA MWANAUME
MWINGINE AMBAYE ALIKIMBIA BAADA YA MTUHUMIWA
KUMKUTA NYUMBANI KWAKE.
MUME WA MAREHEMU AMBAYE KWA SASA NI
MYUHUMIWA MARA BAADA YA KUMSHAMBULIA NA
KUMUUA MKEWE ALIAMUA KUJICHOMA TUMBONI NA KITU
CHENYE NCHA KALI AMBAPO ALIPATA MAUMIVU MAKALI
NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE KWA MATIBABU. UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAKAMILISHWA NA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.
MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI
NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA
MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KUELEKEA SIKUKUU YA PASAKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA
NA VYOMBO VINGINE VYA USALAMA LIMEJIPANGA VIZURI
KUHAKIKISHA SIKUKUU YA PASAKA INASHEHEREKEWA
KWA AMANI NA UTULIVU.
LINASISITIZA WANANCHI KUJIEPUSHA NA MISONGAMANO ISIYO YA LAZIMA KWANI ADUI WETU MKUBWA KWA SASA NI VIRUSI VYA CORONA (COVID 19), LAKINI JESHI LINATOA ONYO JUU YA WATU WANAOPANGA KUJARIBU HATA KUWA KWENYE NAFASI YA KUTAKA KUTEKELEZA UHALIFU KWAMBA ATAKAEJARIBU JESHI HALITASITA KUMKAMATA KABLA NA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA
KUWASHUKURU WANANCHI WOTE WANAOENDELEA
KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI
WAKAMATWE KABLA YA MATUKIO NA LINAENDELEA
KUJIELEKEZA KATIKA MFUMO WA KIMAADILI WA
KUTOTOA SIRI YA WATOA TAARIFA. JESHI LINAWATAKIA
SIKUKUU NJEMA YA PASAKA.