Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, akizungumza na watumishi wa Chama mkoani humu jana kwenye kikao kazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Jengo la Makao Makuu ya CCM Mkoa.
Watumishi wa CCM Mkoa wa Mwanza na wilaya zake wakimsikiliza katibu wa Mkoa, Slum Kalli (hayupo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, akiwapiga msasa watumishi wa Chama katika ngazi mbalimbali za mkoa na wilaya (hawapo pichani) katika kikao kazi kuelekea uchaguzi wa wagombea ndani ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu.Watumishi hao ni makatibu wa wilaya, jumuiya na wa kada zingine mkoani Mwanza.Kushoto ni Katibu Msaidizi na Mhasibu wa Mkoa, christina Baldwin, kutoka kushoto wa pili ni Katibu ya UVCCM James Luhende na Katibu wa UWT Mkoa, Mary George kulia.
Watumishi wa CCM MKoa wa Mwanza wakimsikiliza Katibu wa CCM mkoani humu Salum Kalli, wakati wa kikao kilichowahusisha watumishi wote wa mkoa pamoja na wilaya zake saba za Ukerewe, Nyamagana, Ilemela, Sengerema, Magu, Kwimba na Misungwi. Picha zote na Baltazar Mashaka