Wafanyabiashara wakiendelea na ujenzi wa vibada vyao sokoni humo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha Na Ahmed Mahmoud Arusha Serikali mkoani hapa imeimarisha Ulinzi na Usalama wakati zoezi zima la kuweka miundombinu na hatimaye ugawaji wa maeneo kwa wafanyabiashara katika soko la Samunge lililoungua Moto hivi karibuni jijini Arusha. Kwa muktadha huo wafanyabiashara wamekutwa wakiendelea na ujenzi wa vibanda ili kuanza biashara huku pilika zikiendelea za ujenzi kwenye maeneo waliogawiwa kwa usimamizi wa viongozi wao na kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa. Akiongea wakati wa zoezi la ugawaji Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Arusha Koka Moita alisema kuwa ulinzi umeendelea kuimarishwa na maagizo ya mkuu wa mkoa wa Arusha yanaendelea kutekelezwa na hakuna mtu hata mmoja aliyeleta rabsha. Alieleza kwamba hadi wanamaliza zoezi hilo la ugawaji wa maeneo kwa ajili ya ujenzi teyari maeneo yote yaliotengwa kwa kugaiwa yamesimamiwa na Sasa wanaanza ujenzi na kila mmoja atapata mgao wa mabati chini ya usimamizi wa jeshi la polisi. “Zoezi zima limenda vizuri hakuna tukio lolote la uvunjifu wa Amani lililoripotiwa hadi Sasa hivyo shughuli za ujenzi zinaendelea kwa Amani na utulivu chini ya usimamizi wa kamati ya ulinzi na Usalama tukiongozwa na Mkuu wa mkoa kwa siku zote Tatu” Kwa Upande wake Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Arusha Yusuph Semtana alisema maagizo waliyotoa wanashukuru yametekelezwa kwa asilimia zote. Aidha alieleza kuwa ili kuweza kukabiliana na majanga pindi yanapotokea sokoni humu ni muhimu kuweka njia kwa kugawanya maeneo manne huku miundombinu ya barabara ikiwemo katikati jambo amabalo litasaidia kuingia na kuzima Moto tofauti na awali kilikuwa na msongamano usiopitika. Alisema uwepo wa njia hizo unasaidia kuweza kuzima Moto na kuondoa changamoto iliyojitokeza wakati wa kuzima Moto uliowaka sokoni humo na kuunguza sehemu kubwa ya soko hilo. Nae Kiongozi wa wamachinga mkoani hapa Amaeendelea kuishukuru Serikali kwa kuwa nao bega kwa bega katika kipindi chote Cha janga la Moto hadi wanafikia siku ya Leo kwenye ujenzi Alisema wanaomba salamu zao zimfikie mh Rais Dkt.John Magufuli kwani wakati wote ameonyesha mapenzi ya kuwabeba watu wa kada ya chini licha ya uwepo wa Ugonjwa wa Corona yeye amekuwa anajali zaidi shida za watanzania wanyonge wa nchi hii. Akaahidi kuhakikisha wanasimamia maelekezo ya Serikali katika kukabiliana na Ugonjwa Covid 19 katika maeneo ya wamachinga ili kuendelea na Juhudi za Serikali kuutokomeza Ugonjwa huo katika maeneo yao watafuata utaratibu wa uwekaji wa maji ya kutiririka na sabuni sanjari na vitakasa Mikono. Matukio haya yanakuja Mara baada ya hivi karibuni Soko hilo Majira ya Usiku kuungua Moto na kuteketeza eneo kubwa la soko hilo huku wafanyabiashara kadhaa wakiunguliwa na Moto bidhaa zao zote hali iliyopelekea mfanyabiashara mmojawapo kufariki dunia baada ya kukuta maduka yake yameungua Moto. |