Home Mchanganyiko RC MAKONDA AKAGUA MRADI WA TARURA KINONDONI

RC MAKONDA AKAGUA MRADI WA TARURA KINONDONI

0

……………………………………………………………………………

Na Magreth Mbinga

Wananchi wanaingia hasara kwa kukwepa majukumu yao huku mambo yakienda tofauti wanaanza kuilalamikia serikali ili iweze kupatia msaada.

Amesema hayo leo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaaam Mh Paul Makonda wakati akikagua mradi wa TARURA katika eneo la Kinondoni shamba ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya TARURA na wananchi wa eneo hilo.

Pia amewataka wananchi kuacha kujifanya wajuaji wakati tatizo linapokuwa kubwa kwasababu wakati watu wanaingia katika eneo la mradi ambalo hawatakiwi kuvamia.

Vilevile amewataka wananchi kufanya kazi huku  wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona wasikae ndani watafute hela ili wasije wakafa na njaa.

“Tokeni ndani mkafanye kazi Corona isiwe kigezo cha kujifungia ndani tumepambana na magonjwa mengi ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine tufanye kazi huku tukichukua tahadhari’amesema Makonda.

Aidha  Makonda amekukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA katika wilaya ya Ilala na Kinondoni kujua maendeleo ya miradi hiyo.

“Barabara ni ahadi ya muda mrefu ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ijengwe kutoka makao makuu wa Bakwata hadi Biafra”amesema Makonda.

Hatahivyo amepokea taarifa ya mgogoro kutoka kwa wananchi wa eneo lile kwa kutaka kuvunjiwa nyumba zao bila kupata fidia na walio lipwa wapo na hawajipotiwa na barabara hiyo.

Aidha amewataka wananchi kuwa atatuma kamati yake ifanye ukaguzi na wataanza jumatatu ili walete majibu kamili ili mradi huo uende kwa haraka .