Home Mchanganyiko BODI YA NISHATI VIJIJINI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TAA ZA BARABARANI...

BODI YA NISHATI VIJIJINI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TAA ZA BARABARANI WILAYA YA RUANGWA

0

………………………………………………………………………………………………

Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Nishati Vijijini imekagua utekelezaji wa mradi wa kujenga taa za barabarani katika Halimashauri ya Wilaya ya Ruangwa na kushauri Halimashauri hiyo kuchukua tahadhari ya usalama wa nguzo za taa hizo.

Ushauri huo umetolewa tarehe 03/04/2020 na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Styden Rwebangira wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini katika Mkoa wa Lindi. “Mfikirie jinsi gani ya kukinga nguzo za taa zisigongwe na magari na kuzilinda dhidi ya wizi. kwa mfano mnaweza angalia maeneo hatarishi kama vile kwenye kona na kutafuta njia ya kukinga nguzo hizo zisigongwe na magari”

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Ruangwa Rashid Oga Namkulala alisema mradi huo umeongezewa muda hadi tarehe 30 Mei, 2020 badala ya tarehe 31 Machi 2020 ambapo ulitakiwa ukamilike kutokana na ugonjwa wa homa ya mafua ya virusi vya Corona ambao umesababisha vifaa kutoka China kuchelewa kuletwa nchini.

Kamati ilielezwa kuwa jumla ya nguzo za taa 88 kati ya 187 zimeshajengwa

Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa Halimashauri hiyo na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).