Sehemu ya Soko la Samunge linavyoonekana Mara baada ya kufanyiwa Usafi baada ya kuteketea kwa Moto mwishoni mwa wiki iliyopita picha Zote na Ahmed Mahmoud Arusha
|
Muonekano wa Soko la machinga Samunge kama lilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha leo leo majira ya jioni wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo |
|
Pichani ni eneo la Magharibi la soko la Samunge lilivyoonekana jioni hii baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutoa Mabati Mia Saba ya kuanza ujenzi wa vibanda Kesho picha na Ahmed Mahmoud Arusha. |
|
Sehemu ya Mashariki mwa soko la Samunge |
|
Sehemu ya vibanda vilivyo pembezo mwa soko hilo wakiendelea na biashara wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo |
|
Waandishi wa habari wakitekeleza majukumu yao kama walivyokutwa na kamera ya matukio alasiri hii jijini Arusha |
|
Greda likiendelea na kazi ya kusawazisha eneo la soko hilo |
|
Biashara ikiendelea sokoni humo jioni ya leo |
|
Wafanyabiashara wadogo wakiendelea na biashara yao sokoni humo |
|
Wamachinga wakihamisha sehemu ya mabaki ya vibada kwa kutumia mkokoteni kama walivyokutwa na kamera ya matukio jioni ya leo jijini Arusha |
|
Biashara inaendelea baada ya Serikali ya wilaya kufunga barabara kuwapisha wafanyabiashara hao kujipatia riziki baada ya soko la Samunge kuteketea kwa Moto mwishoni mwa wiki iliyopita |
|
Sehemu ya wafanyabiashara wa soko la Samunge wakijongea kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo jioni ya leo jijini Arusha |
|
Umati wa wafanyabiashara Soko la Samunge wakisogea teyari kumsikiza Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Arusha alasiri ya leo jijini Arusha |
|
Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo |
|
Umati wa wafanyabiashara |
|
Wafanyabiashara wakimsiliza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo |
|
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa pichani kwenye ziara ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo |
|
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katikati ya Kamati ya Ulinzi na Usalama akiongea na wafanyabiashara ndogo ndogo wa soko la Samunge jioni ya leo jijini Arusha |
|
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari wakifuatilia tukio hilo |
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mwenye Kofia ya kapelo akipata maelezo kabla ya kuzungumza na wafanyabiashara hao jioni ya leo jijini Arusha |
|
Gambo akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen mwenye miwani kwenye ziara ya kukagua madhara na kutangaza kuanza kwaujenzi wa soko hilo kesho |
|
Viongozi wakiteta jambo kabla ya kuongea na wamachinga wa soko la Samunge |
|
Sehemu ya Mabati mia Saba yaliotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kukabidhi kwa Mwenyekiti wa wamachinga hao ikiwa ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa soko hilo kesho. |
|
Wananchi na wafanyabiashara hao wakifuatilia makabidhiano hayo jioni ya leo kwenye soko la Samunge |
|
Add caption |
|
Add caption |
|
Add caption |
|
Add caption |
|
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitolewa Mara baada ya kumaliza ziara huku wananchi wakimsindikiza kwa shangwe hadi kupanda gari na kuzuia msafara wake kwa muda baada ya kukoshwa naye kuwaruhusu kuanza kwa ujenzi upya kesho picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametoa jumla ya mabati 700 kwa wafanyabiashara wadogo waliounguliwa na vibanda vyao kwenye soko la Samunge mwishoni mwa wiki iliyopita huku chama cha Mapinduzi kikitoa milion 1.
Akiongea wakati walipofanya ziara kwenye soko hilo akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapa Gambo ameendelea kuwatoa hofu wafanyabiashara hao kuwa hakuna wa kuwaondoa sokoni humu na kuwataka kuanza ujenzi Mara moja ili kuendelea na kazi zao za kila siku kwa kuwa familia zinawategemea.
Amewaambia Rais Dkt.John Magufuli Ameeleza wazi kuwa atakae waondoa ataenda na maji hivyo wao kama Serikali ya mkoa na wilaya wanaendelea kuangalia na kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha kufanya biashara zao bila vikwazo vyovyote.
Alibainisha kuwa atakaa na Taasisi za fedha kuona jinsi ya kuchukuwa hatua za kuwapa nafasi ya kipindi Cha uangalizi wale wenye mikopo na kuwashangaa Taasisi hizo kama wao hawakuona uala hilo hivyo kuwataka wote wenye kudaiwa kufika kwenye ofisi yake na nyaraka zote ili waweze kukaa nao pamoja na Taasisi hizo.
” Ndugu zangu najua mnategemea Sana biashara hizi mkalishe watoto wenu kwani mpatacho ndio kinaenda huko Sasa kesho saa moja nipo hapa kuona shughuli za ujenzi zikiendelea na nilitoka hapa naenda kwa mwenzenu kuona jinsi atakavyo sitiriwa kama Serikali tutahakikisha shughuli hizo zinaenda kwa haraka Sana”
Aliwaambia soko hilo sio la halmashauri ni sehemu ya wamachinga na hakuna wa kuwatoa humo kwa sababu yeyote mwenye kitambulisho Cha machinga anayofursa ya kufanyabiashara Ila asitokee yeyote aliyekuwa hayupo akaingia najua mnajua wote humu.
Alisema kuwa wapo watu ambao wanampango wa kujichomeka hilo halitakubalika hata Mara moja kwa kuwa sehemu hii ni ya wafanyabiashara wa chini nanajuana mwenye ndizi wa pembeni yake anamjua na vilevile mwenye mbogomboga wapembeni yake anamjua anzeni ujenzi Mara moja ili muweze kujipatia kipato Cha kuendesha familia zenu.
“Maisha ya watu wa kipato Cha chini nayajua vizuri Sana saa nyingine najua mnategemea kuendesha maisha kwa kipato unachopata siku hiyo ndio maana mh.Rais amaeendelea kusisitiza tufanye kazi kwani anajua hali zenu wanyonge nasi tutaendelea kusimamia kuhakikisha mnafanyakazi zenu kwa Uhuru bila kubughuziwa”
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen amesema kuwa Serikali inatakiwa kuonyesha jambo kuweza kuangalia namna nzuri ya kuwasaidia wahanga hao wa Moto ili waweze kuendelea na ufanyaji wa biashara kwa haraka badala ya kuendelea kuchukuwa muda mrefu.
Alisema watu hao wanategemewa na familia zao na kazi hiyo ndio inaendesha maisha yao ya kila siku najua hata leo familia inasubiria na wengine humu wamelala njaa na Taasisi za fedha zanawadai hivyo busara ya Serikali inahitajika Sana kipindi hicho kuchukuwa hatua za haraka.
Nae Mwenyekiti wa wamachinga mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa wamachinga Soko la Samunge wameendelea kuishukuru Serikali ya wilaya na mkoa kuendelea kuwatoa kwenye hofu waliyokuwa nayo awali kuondolewa na kuchelewa kwa shughuli zao za kujipatia riziki zao.
Walisema kuwa Serikali ya mkoa wanaendelea kuishukuru na wampelekee salamu zao Rais wa Jamhuri ya Muungano huku wakisema waliye Koka naye Moto ndio wataota nae hivyo wao wapo nae siku zote kwa kuwa amewaonyesha kuwajali wakati wa shidana kujua hali zao nao kujiona ni sehemu ya watanzania