Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Meru wakifuatilia kikao chao kikiendelea kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo na kupendekeza halmashauri hiyo kuwa na hadhi ya mji picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha |
Kikao kikiendelea na kupendekeza halmashauri hiyo kuwa ya Mji badala ya Sasa wilaya. |
Mwenyekiti wa halmashauri ya Meru Akiongoza kikao cha baraza la madiwani kwenye halmashauri ya Meru akiwa na Mkurugenzi wake Emmanuel Mkongo |
Diwani Malula Mafie akichangia kwenye kikao hicho Cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Meru.picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha |
Arusha.Baraza la madiwani wilaya ya Meru wamepitisha mapendekezo ya kuipandisha hadhi halmashauri hiyo kuwa halmashauri ya mji ili kuweza kuwafikia wananchi katika kutoa maoni yao na baadaye katika kikao cha baraza la washauri mkoa(rcc) na kufikishwa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi).
Akizungumza mmoja wa madiwani hao kutoka kata ya maji ya chai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya uchumi,ujenzi na mazingira, Anderson Pallangyo alisema mapendekezo ya kuipandisha hadhi halmashauri ya meru kuwa ya mji yalianza kujadiliwa katika kamati yake baada ya wataalamu kuleta wazo hilo kwa kutaka kupandisha hadhi mji wa Usa kutoka kwenye mamlaka ya mji mdogo kuwa mamlaka kamili ya mji.
Pallangyo alisema “baada ya wataalamu kuleta wazo hilo hawakukubaliana baada ya kuupitia nakuona kwamba hautafaa hivyo wakawaomba warekebishe kwani wazo hilo lilikuwa linawatenganisha wao na kuongezewa kazi za uendeshaji wa halmashauri.”
Alisema lakini mpango huo wa kupandisha hadhi halmashauri hiyo kuwa ya mji ni mzuri kwani utawanufaisha wananchi kuwekeza maeneo yao katika biashara nakupata faida kwa wawekezaji kutokana na mpangilio mzuri wa mji wataongozwa na sheria namba 8 ya mwaka 1982 ya mipango miji.
“Tutaenda kuchukua maoni ya wananchi ili mchakato huu usonge mbele kama sheria inavyosema za upandishaji hadhi mji ingawa changamoto inaweza tokea kwa baadhi ya wananchi kwa kuona maeneo yao kutengwa sehemu ya mijini lakini anaweza elimishwa na kuweza kubadilisha matumizi,” alisema.
Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Meru,Emmanuel Mkongo alisema baada ya baraza la madiwani kuridhia wataenda kuchukua maoni ya wananchi ili waweze kujadili katika vikao vya ndani na baadae mapendekezo hayo kupelekwa katika kikao cha RCC ili kuweza kujadiliwa kwa ajili ya kufikishwa Tamisemi.
“Halmashauri hii ikipandishwa hadhi baadhi ya mambo yatabadilika na hata vijiji vichache vitakuwa mitaa na wananchi watanufaika kupitia mabadiliko hayo,” alisema Mkurugenzi Mkongo.
Hata hivyo Makamo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa Malula,Nelson Mafie alisema mpango huo ni mzuri kuliko wa awali hivyo ni vyema wakazingatia hicho wanachopitisha kisijeleta shida kwa wananchi hivyo ni vizuri wakaendelea kupata elimu ya umuhimu wa kupandisha hadhi halmashauri ya wilaya kuwa ya mji.