Mkurugenzi wa Tiba (MOI) Dkt. Samwel Swai (kulia) akipokea baadhi ya vifaa kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya EAA Josiah Benedict leo katika viwanja vya (MOI) jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Tiba (MOI) Dkt. Samwel Swai akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya EAA Josiah Benedict pamoja na baadhi ya wafanyakazi wengine waliohudhuria warsha ya makabidhiano leo katika
viwanja vya (MOI) jijini Dar es Salaam
******************************
Kampuni ya EAA Co. Ltd ya nchini Japan imetoa msaada wa viungo bandia vyenye thamani ya Shilingi milioni 80.9 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) leo Jijini Dar es Salaam.
Akipokea msaada huo, Mkurugenzi wa Tiba (MOI) Dkt. Samwel Swai amesema kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa matibabu ya wagonjwa wenye ulemavu wa miguu naa mikono.
Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya EAA Co. Ltd, Josiah Benedict amesema wameguswa na changamoto zinazowakabili watanzania ndiyo maana wameamua kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.
Msaada huo unatokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania Japan kwa kushirikiana na Watanzania waishio nchini Japan.