Home Mchanganyiko Mbunge  wa Arumeru Mashariki awataka wazazi nchini kuchukua tahadhari ya virusi vya...

Mbunge  wa Arumeru Mashariki awataka wazazi nchini kuchukua tahadhari ya virusi vya korona kwa watoto wao.

0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,John Pallagyo akizungumza na viongozi wa umoja  wa wanawake wilaya ya Meru  alipotembelea mradi wa umoja huo wilayani Arumeru mkoani Arusha ambao wanatarajia kuweka mashine ya kusaga na kukoboa pamoja stationari.(Happy Lazaro).
***********************************
Happy Lazaro,Arusha.
Mbunge wa Arumeru Mashariki ,John Pallagyo amewataka wazazi kote nchini kusimama kikamilifu katika nafasi zao katika kuwalinda watoto wao wakiwa likizo wasidhurure ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya korona.

Ameyasema hayo janawakati akizungumza katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la  Umoja wa wanawake wilaya ya Meru lililopo katika kata ya Poli wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Pallagyo alisema kuwa,hivi sasa nchi inapambana kikamilifu kuhakikisha wananchi wanafuata sheria na kanuni ili kuepukana na maambukizi ya virusi hivyo ambavyo vimekuwa ni tishio ndani na nje ya nchi,hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anajikinga na kuwakinga wengine kila mmoja kwa nafasi yake.
Hata hivyo  aliwataka wazazi kuhakikisha wanaiunga mkono serikali kwa kufuata sheria na taratibu za nchi zilizowekwa hasa katika kipindi hiki ambacho watoto wapo likizo ili wasiambukizwe.
Alifafanua kuwa,wakina mama ndio wenye familia zetu,hivyo aliwataka kuwabana watoto wasiwe wanazurura hovyo ,ili kwa pamoja wasimame imara katika janga hili kuhakikisha watoto wetu wanafuata sheria na miongozo ya nchi.
Naombeni Sana jamani mhakikishe mnachukua tahadhari na kuwalinda watoto wenu wakiwa likizo kwani hivi sasa wapo mikononi mwenu ili waepukanae na ugonjwa huo alisema Mbunge huyo.
Alisema kuwa ,mwaka jana  uongozi wa UWT wilaya ya Meru    walimwomba awasaidie kujenga jengo hilo kwa ajili ya mradi wao wa kusaga na kukoboa pamoja na ofisi ya stationery.
Alisema kuwa, kumalizika kwa mradi huo kutawasaidia Sana wanawake hao kuweza  kujitegemea wakati wakiendelea na kazi ya kukijenga chama.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Meru,Julieth Maturo alisema kuwa,kukamilika kwa mradi huo kutasaidia Sana  wanawake hao kuweza kujitegemea na kuondokana na kuwa tegemezi.
Alisema kuwa,jengo hilo ambalo hivi sasa lipo hatua ya lenta limeshagharimu kiasi cha shs 11 milioni ambapo hadi kukamilika linatarajia kutumia kiasi cha shs 18 milioni,na wataweza kufungua mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa,pamoja na stationary.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa UWT wilaya ya Meru, Elizabeth Hayuma alimshukuru Mbunge huyo kwa namna alivyowasaidia kwani kwa pamoja wanashirikiana na mbunge huyo katika kukamilisha ujenzi huo.