Home Mchanganyiko JAJI KIONGOZI ATAKA KESI ZA JINAI KUSIKILIZWA MFULULIZO

JAJI KIONGOZI ATAKA KESI ZA JINAI KUSIKILIZWA MFULULIZO

0

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi (katikati) akikagua  leo ujenzi wa  jengo   la Kituo  cha Mahakama Jumuishi  cha  Utoaji Haki (IJC) kilichopo Kinondoni. Kituo hicho  kinajumuisha Mahakama Kuu,  Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya, Mahakama   ya Mahakama Mwanzo,   zikiwemo ofisi za wadau wote wa Mahakama.

Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo akitoa (kushoto)taarifa ya utendaji wa Mahakama hiyo kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi( ambaye hayupo pichani).

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi (kulia) na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam( kushoto) (katikati) akinawa mikono mara ikiwa ni hatua ya kupambana na maambukizi  ya virusi  vinavyosababisha vya ugonjwa wa Corona  baada ya kuwasili  leo katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam. Jaji Kiongozi yuko katika ziara maalum ya kikazi kwenye Mahakama Kuu ya  Kanda   ya Dar es Salaam.

Picha na Magreth Kinabo- Mahakama

*******************************

Na Magreth Kinabo- Mahakama

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Eliezer Feleshi, amewataka Mahakimu kusikiliza kesi za jinai kwa mfululizo ili  ya kuweza kupunguza msongamano  wa mahabusu,  na kuepukana na maambukizi ya Virusi Corona.

Jaji Kiongozi alitoa agizo hilo leo mara baada ya kutembelea mahakama mbalimbali za Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya ukaguzi maalum.

“Anzeni kusikiliza kesi za jinia mfululizo, itasaidia tusiwe na msongamano wa mahabusu, na wale wanaostahili dhamana  wapewe,  hatua hii itatuwezesha kujikinga na maambukizi ya  virusi vya Corona, alisema Jaji Kiongozi.

Aidha Jaji Kiongozi amewataka  watumishi wa Mahakama kuendelea kuepukana na vitendo vya rushwa na kuzingatia maadili ya kazi zao.

Dkt. Feleshi  alizipongeza Mahakama za Mwanzo kutokuwa na mlundikano wa mashauri.

Jaji Kiongozi ameanza ziara ya ukaguzi maalum katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo inatarajiwa kumalizika Aprili 3, mwaka huu.

Katika ziara hiyo Jaji Kiongozi alikagua ujenzi wa ujenzi wa  jengo   la Kituo  cha Mahakama Jumuishi  cha  Utoaji Haki (IJC) kilichopo Kinondoni. . pia alikagua  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mahakama ya  Wilaya Kinondoni na Mahakama za Mwanzo za Sinza, Kinondoni,Kaw. Kimara, Magomeni na Kariakoo.