Baadhi ya Maduka Jijini Dar es Salaam yakitekeleza utaratibu uliowekwa na Wizara ya Afya kwa kuweka kitakatisha mikono (Sanitizer) na ndoo ya maji katika maeneo ya shughuli zao ili kuweza kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Baadhi ya Wateja katika maduka yaliyopo maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam wakinawa mikono kwa kutumia maji safi na salama ili kuweza kuhudumiwa.
*************************
NA EMMANUEL MBATILO
Baadhi ya Wakazi wa Jijini la Dar es Salaam wameanza kutekeleza agiza kutoka kwa Wizara ya Afya namna ya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo katika maeneo ambayo shughuli za kila siku zinafanyika wameweka ndoo yenye maji safi pamoja na vitakatisha mikono (Sanitizer) kwaajili ya kujikinga na maambukizi hayo.
Wakizungumza katika nyakati tofautitofauti wakazi hao wamesema ni bora wajitambue wao kama wao ili kuweza kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwani ni ugonjwa hatari na unaua.
Bw.William Lyimo mkazi wa Ubungo Msewe Jijini Dar es Salaam amesema kuwa wananchi wanatakiwa watambue umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya Virusi hivyo ili kuweza kuondokana na maambukizi hayo.
“Viongozi wa Serikali wakiwemo Wizara ya Afya, Vyombo vya Habari, Taaisisi mbalimbali za Afya wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona kwa wananchi wake lakini mpaka sasa wananchi wengi wameenza kuelewa na kuaanza kuchukua hatua”. Amesema Bw.Lyimo.
Aidha Bw.Lyimo ameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali hasa vijijini kuelewa ni madhara gani yanaweza kuitokeza pindi Maambukizi ya Virusi Vya Corona vikimpata mtu na namna ya utoaji taarifa kwa mtu ambaye ana dalili za Maambukizi hayo.
Nae Bi.Maria Julius ambaye ni Mkazi wa Kimara temboni amesema kuwa elimu ambayo inatolewa na Serikali kwa wananchi wake kujikinga na Maambukiz ya Virusi vya Corona haifuatwi kwa wananchi ambao wapo majumbani kwao kwani wamekuwa wanachukulia kawaida.
“Ukiingia katika jamii hasa majumbani kwenu wengi wamekuwa hawafuati utaratibu wa kujinga na maambukiz ya Virui vya Corona ila katika maeneo ambayo shughuli nyingi za kijamii zinafanyika hasa kwenye masoko wamejitahidi kuweka sehemu maalumu ya kujisafisha mikono kabla ya kuhudumiwa, hii ni hatua kubwa mno hasa katika kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona”.Amesema Bi.Maria.
Mpaka sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa idadi ya walioambukizwa na Virusi vya Corona imefika watu 13.