Home Mchanganyiko VIJANA WATAKIWA KUWA WAZALENDO WA NCHI NA KUACHA KUJIINGIZA KATIKA UHALIFU

VIJANA WATAKIWA KUWA WAZALENDO WA NCHI NA KUACHA KUJIINGIZA KATIKA UHALIFU

0

******************************

Ikiwa imebakia miezi kadhaa Tanzania kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa Nchi ikiwemo Raisi,Madiwani,na Wabunge Vijana wamepaswa kuwa wazalendo wa Nchi yao kwa kuacha kujiingiza katika viashiria vya uvunjifu wa amani ili kusaidia kuepukana na migogoro itakayopelekea uvunjifu wa Amani.

Rai imetolewa leo Jijin Dar es salaam na Rais wa Afrika Mshariki wa Shirika la Elimu la Amani aifa WILSONI MUNGUZA katika mkutano na wanahabari.

Akizngumza katika Mkutano huo Bw.Munguza amesema machafuko mengi yanayotokea hasa Nchi za jirani asilimia kubwa hutokea baada Uchaguzi baadhi ya viongozi wa siasa kutoridhika na matokeo ya Uchaguzi hivyo wengine kuwanunua vijana wafanye vurugu ikiwemo kuandamana nao wasikubali kununuliwa kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria na utaratibu uvunjifu amani.

“Vijana wasikubali kununuliwa kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria na utaratibu ikiwamo uvunjivu wa amani vijana wawe na uzalendo kutunza amani ya nchi hili jukumu letu sote waache kufanya mambo ambayo hayana faida katika kuleta maendeleo nchini”. Alisema Bw.Munguza.

Hata hivyo Bw.Munguza amewaasa Viongozi wa kidini wafanye kazi zao na waache kutumia muda wao kuhubiri siasa na kuwapigia kampeni baadhi ya viongozi wa kisiasa.

“Nawaomba viongozi wa dini wasitumiwe na wanasiasa kuleta mkanganyiko katika jamii kwa kuchanganya uanasiasa na masuala ya kidini, inatakiwa wasimame kwenye majukumu yao ikiwemo majukumu ya kuleta amani katika nchi.” Alisema .Bw.Munguza.

Kwa upande wake Afisa Elimu Taifa Shirika la Elimu ya Amani, RUKIA MANDINDI amesema wanawake wanapaswa kuwa makini kuhamasisha amani kwani kujitolea machafuko waathirika wakubwa ni wanawake na watoto ambao hivyo ni budi kutojihudisha kwa kupokea rushwa aina yeyote na wawe makini kupokea maelekezo yote ili kuepukana na machafuko yatakayopelekea uvunjifu wa amani.

“Wanawake ni chachu katika kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani hivyo, nawaomba wanawake wenzangu kutokushiriki katika hatua mbalimbali za uvunjivu wa amani waache kupokea rushwa, wawe makini wapokee maelekezo kwa mujibu kutoka Serikalini katika kuelekea Uchaguzi.” Alisema Rukia.

Aidha wito umetolewa kwa Watanzania kuendelea kulinda amani iliyopo ambayo waasisi Mwalimu Julius Nyerere na Amani Karume wakipoteza kuirudisha itagharimu hata kumwaga damu Kama wanavyohangaika Baadhi ya Nchi ikiweo Libya,Iraki,Burundi.