************************
Hadi kufikia mwezi wa tano kutakuwa na madiliko makubwa kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya mwendo kasi inayojengwa katika Wilaya ya Temeke.
Amezungumza hayo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda katika ziara yake ya kukagua mradi huo .
Pia amesema barabara hiyo ni ndefu ambayo itafika stesheni hadi bandari ili wageni watakao toka Zanzibar wawezekusafiri na itafika hadi Magomeni .
“Ujenzi umechelewa kwasababu ya mazingira ya mvua na mabadiliko ya kuongeza vituo mpaka sasa kuna vituo ishirini na tisa ili kupunguza hadha ambayo wanaipata watu wa Kimara”amesema Makonda.
Vilevile amesema mkandarasi amelazimika kujenga barabara za zarula ili wasikwamishe shughuli za usafiri kwasababu watu wengi wanatumia barabara hiyo na abiria wa kusini pia.
“Mkandarasi amesema changamoto zote wamekwisha kufanyia kazi na anatumaini wiki ijayo wataongeza sehemu ya pili “amesema Makonda.
Sanjari na hayo Makonda amewataka wananchi wanaokaa bondeni wachukue tahadhari kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwezekana wahame maeneo hayo hatalishi.
Hatahivyo amesema Serikali imepokea pesa isiyopungua Bilioni 200 kwaajili ya kufanya mabadiliko ya eneo la mto Msimbazi ili liwe sehemu ya mapumziko .
“Wananchi wawe wavumilivu viongozi wao wanafanyia kazi changamoto wanazokutana nazo katika mto Msimbazi tutabadilisha kuwe kama Paris”amesema Makonda.