Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani akiwa na mkuu wa
wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alipofanya ziara katika bwawa la Mtera.
Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na
waandishi wa habari mkoa wa Morogoro na Iringa katika vituo vya kuzalishia umeme vya Kidatu na Mtera akitoa katazo la kuwepo kwa mgao wa umeme hapa nchini.
Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani akikagua
miundombinu ya Dalaja la mto Kilombero kabla ya kufika katika kituo
cha kuzalisha umeme cha kidatu Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nishati Dkt Medadi Kalemani akikagua mitambo
katika kituo cha kuzalishia umeme cha kidatu Mkoani Morogoro,akiwa katika ziara yake ya kukagua vituo vya kuzarisha umeme hapa nchini.
****************************
Na Farida Saidy Morogoro.
Kufuatia Baadhi ya Mikoa hapa nchini kukosa umeme wa uhakika Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amefanya ziara ya kukagua vituo vya kuzalishia umeme Kidatu Mkoani Mororgoro ikiwa na kituo cha Mtera Mkoani Iringa kwa lengo la kubaini chanzo cha kukosekana na kwa umeme katika mikoa hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Waziri Kalemani Mara baada ya kutembelea vituo hivyo amewata viongozi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO kuacha tabia ya kutoa mgao wa umeme kwa wananchi, na kusema kuwa Tanzania inaumeme wakutosha hivyo hatarajii kuona kuna mkoa hauna umeme kwa kigezo cha upungufu wa
umeme.
Hata hivyo Waziri Kalemani ikiwa katika kituo cha uzalishaji wa umeme Mtera mkoani iringa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt.Tito Mwinuka Kuhakikisha anamchukulia hatua mfanyakazi Abubakari kwa kosa la kuagiza mkoa wa Mwanza uwe na mgao wa umeme bila sababu za msingi.
“Usipomchukulia hatua huyu mfanyakazi anaeitwa Abubakari basi Mimi nitajua nani wa kumchukulia hatua kwa kuwa tatizo hilo kwa Abubakari limekuwa likijirudia mara kwa mara” alisema Waziri Kalemani.
“haiwezekani mtu mmoja anaamua kutoa maagizo ya kuwepo mgao wakati hakuna tatizo lolote lile”alisema Waziri Kalemani .
Alisema serikali imejenga nyumba za wafanyazi pale ubongo kwa ajili ya uangaliangalizi wa mwenendo wa umeme nchi nzima lakini bado wafanyakazi wanakaidi kukaa hapo jambo linalopelekea ufanisi wa kazi
kuwa hafifuBkatika hatuan nyingine Dkt. Kalemani alitoa tahadhari kwa wananchi waliokaribu na mto ya Ruaha mkuu pamoja na kilombero kuchukua tahadhari ya kundoka katika maeneo hayo hususani katika kipindi hiki
ambacho maji yanafunguliwa katika mabwawa ya kuzalishia umeme.
“tumeona ni muhimu kutoa tahadhari kwa Wananchi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, kwa kawaida Bwawa la Mtera kulijaza huchukua miezi 3 hadi 4 kwa mvua za masika, lakini kwa kipindi hiki mvua za vuli zimekuwa nyingi ndani ya mwezi mmoja hivyo kina
kimeongezeka”, alisema Dkt. Kalemani.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara kwa wananchi kwa lengo la kuwaokoa na madhara ambayo wanaweza kuyapata kipindiki
cha mafuriko hasa wale wanaofanya shughuli katika bwawa la Mtera na kandokando ya mto Ruaha.
katika hatua nyingine Kasesela alimuomba waziri kusaidia kuharakisha ujenzi wa daraja jipya ambalo michoro yote imekamilika ila fedha bado hazijapatika kwa lengo la kuliokoa daraja lililopo kutokana na magari yanayopita hapo yanauzito mkubwa sana.