Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF- Net), Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Maria Nzuki akimkabidhi msaada wa unga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa
Wilaya hiyo waliopata maafa ya mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni. Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania ulikabidhi msaada wa unga kilo 1000, Maharage kilo 500, mafuta ya kula lita 120, sukari kilo
100 pamoja na sabuni box 18.(Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo akimkabidhi mfuko wa unga mkazi wa Wilaya hiyo ambaye ni miongoni mwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni kushoto ni Mwenyekeiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania,(TPF Network)
DCP Maria Nzuki. Mifuko hiyo ya unga ni sehemu ya msaada iliyokabidhiwa na Mtandao wa Polisi wanawake Tanzania (TPF-Net) Machi 19, mwaka huu. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF- Net), Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Maria Nzuki akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo mara baada ya kumkabidhi msaada kwa ajili ya kuwapatia wananchi wa Wilaya hiyo waliopata maafa ya mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi).
****************************
Na Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania, (TPF Network) Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Maria Nzuki ameitaka jamii kuguswa na kuwasaidia wakazi wa Wilaya ya Rufiji waliopata maafa ya mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni katika Wilaya hiyo na
kupelekea baadhi ya wakazi wake kukosa makazi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji.
Aliyasema hayo wakati wa kukabidhi misaada mbalimbali kwa wakazi wa Rufiji kwakuwa mafuriko waliyoyapata yameleta hasara kubwa kwao ikiwemo na kupoteza makazi sambamba na kusimama kwa shughuli za uzalishaji mali kwa jamii.
DCP nzuki alisema Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania umetoa msaada wa unga kilo 1000, maharage kilo 500, mafuta ya kula lita 120, sukari kilo 100 pamoja na sabuni box 18 kwa ajili ya wahanga waliopata mafuriko.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo ameushukuru Mtandao huo kwa msaada waliotoa na kusema kuwa msaada huo utawasaidia sana kwa kuwa zaidi ya Hekta 4000 za mazao zimesombwa na maji hivyo kuongeza mahitaji ya chakula kwa wakazi waliokumbwa na mafuriko.