Home Michezo YANGA YALAZIMISHWA SARE NA NAMUNGO FC KWENYE UWANJA WA MAJALIWA

YANGA YALAZIMISHWA SARE NA NAMUNGO FC KWENYE UWANJA WA MAJALIWA

0

****************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Yanga imeweza kulazimishwa sare ya 1:1 na timu ya Namungo Fc ambayo ilikuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majaliwa.

Yanga ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Tariq Saleh mnamo dk.6 ya mchezo akimalizia krosi iliyopigwa na Juma Abdul.

Baada ya mapumziko Namungo ilirudi kipindi cha pili ikionesha hali ya kutaka kurudisha goli hilo kwani walifanya mashambulizi ya mara kwa mara, hata hivyo Bigirimana Blaise aliweza kufanikiwa kusawazisha goli mnamo dk.62.

Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi mechi iliisha sare ya 1:1.