Home Mchanganyiko Waziri Biteko Aagiza Kupitiwa Upya Nyaraka za Fidia Mgodi wa Nyakamtwe Njombe

Waziri Biteko Aagiza Kupitiwa Upya Nyaraka za Fidia Mgodi wa Nyakamtwe Njombe

0

***********************************

NJOMBE

Waziri wa madini Dotto Biteko ameagiza kupitiwa upya vielelezo vya vifidia ambazo zililipwa na muwekezaji katika mgodi wa GRANITE wa Nyakamtwe Quarry ili kuepusha mgogoro baina ya muwekezaji na wananchi ambao wamevamia eneo hilo na kuendelea na ujenzi wa makazi kwa madai ya kumiliki kihalali.

Biteko ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea mgodi na kupokea malalamiko kutoka kwa muwekezaji ambapo amesema ili kumaliza mgogoro huo mkuu wa mkoa huo Chritopher Olesendeka anapaswa kukutana na maafisa ya madini na miamba mkoa,halmashauri ya mji wa Njombe pamoja na muwekezaji wa mgodi wa  NYWAKAMTWE QUARRY ili kupitia upya taarifa za malipo ya fidia kwa watu waliopisha mgodi.

Amesema kupitiwa upya kwa nyaraka hizo kutasaidia kupata ukweli kuhusu kiwango cha fidia na idadi ya watu waliopokea hatua ambayo itasaidia kutatua mgogoro wa wavamizi wa eneo la mgodi huo ambao wanadai wanamiliki kihalali kwani hawakulipwa fidia yeyote.

Awali mkurugenzi wa kampuni ya NYAKAMTWE QUARRY Isaya Mhagama anasema tangu anachukua mgodi huo mwaka 2000 amekuwa akikwamishwa na uvamizi wa watu ambaowamekuwa wakianzisha makazi kwa madai ya kuwa wamiliki halali wa maeneo hayo huku pia matumizi ya mitambo ya kizamani yakitajwa kuwa tatazo kwa maendeleo ya mradi.

Katika hatua nyingine waziri ameonyesha kutoridhishwa na teknolojia ya uchimbaji inayotumiwa na muwekezaji huyo na kisha kumtaka kununua mitambo ya kisasa ili kuepusha upotevu wa madini ambao unajitokeza sasa.