Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiongea na baadhi ya Watendaji Mkoani Shinyanga alipofika Mkoani humo leo kujionea Ofisi za Wizara ya Ardhi zitakazotumika kuifadhi baadhi ya nyaraka za Ardhi Mkoani humo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa maelekezo kwa baadhi ya Watendaji Mkoani Shinyanga alipofika Mkoani humo leo kujionea Ofisi za Wizara ya Ardhi zitakazotumika kuifadhi baadhi ya nyaraka za Ardhi Mkoani humo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akibadilishana na mawazo na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw.Albert Msovera kwa baadhi ya Watendaji Mkoani Shinyanga alipofika Mkoani humo leo kujionea Ofisi za Wizara ya Ardhi zitakazotumika kuifadhi baadhi ya nyaraka za Ardhi Mkoani humo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa maelekezo kwa baadhi ya Watendaji Mkoani Shinyanga alipofika Mkoani humo leo kujionea Ofisi za Wizara ya Ardhi zitakazotumika kuifadhi baadhi ya nyaraka za Ardhi Mkoani humo.
**************************
Na Anthony Ishengoma -Shinyanga
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka Wakurugenzi wa Almashauri zote za Wilaya pamoja na Manispaa ya Mkoa wa Shinyanga kuharakisha upimaji ardhi na utoaji hati za umiliki wa ardhi kwa wananchi ikiwemo mipango miji ili kuongeza mapato ya Serikali na kuepukana na ujenzi holela mkoani humo.
Waziri Lukuvi amesema hayo Mkoani Shinyanga alipofika Mkoani humo kwa lengo la kujionea ofisi mpya zitakazotumiwa na Msajili wa Ardhi pamoja na Kamishina wa Ardhi kutoka Wizara yake kwa lengo la Wizara yake kutoa huduma katika kila mkoa tofauti na awali ambapo huduma hizo zilipatikana Makao Makuu ya Wizara.
‘’Kuanzia sasa hakuna mwananchi masikini kusafiri kutoka Mkoa mmoja kufuata hati mkoa mwingine na sasa Wizara inaweka Ofisi kila Mkoa yenye vifaa vya kisasa vitavyosaidia masuala yote ya mipango miji na upimaji ardhi katika kila Wilaya bila kulazimika kufuata huduma hizo katika makao makuu ya Wizara ya Ardhi’’. Alisema Waziri Lukuvi.
Waziri huyo wa mwenye dhamana ya masuala ya Ardhi hapa Nchini amesema Mkoa wa Shinyanga una hati 15,000 zilizosajiliwa ambazo nyaraka zake zimeifadhiwa na Wizara yake lakini kwasasa zitaletwa na kuhamishiwa Mkoani Shinyanga zikiwemo nyaraka nyingine za mipango miji ya shinyanga zilizokuwepo kabla ya uhuru akiongeza kuwa nazo kwasasa zitaletwa mkoani Shinyanga tofauti na hapo awali zilipokuwa zikiifadhiwa Makao Makuu ya Wizara yake.
Aidha Waziri Lukuvi amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanapima ardhi na kumilikisha wananchi ili waweze kutumia ardhi kama dhamana ya mikopo ya benki ili fedha zitakazopatikana ziweze kuingia katika mzunguko na hivyo kuchochea maendeleo ya mkoa lakini pia iwe hatua muhimu ya kukomesha ujenzi holela na kupanga makazi bora badala ya kuanza kuboresha na kuendeleza miji wakati ujenzi holela ushaanza.
‘’Unapowamilikisha watu ardhi unaongeza pato la serikali litokanalo na kodi ya ardhi lakini pia unawawezesha wananchi kutumia hati ya ardhi kupata mikopo ya benki ambayo uchangia kuingiza fedha kwenye mzunguko na hivyo kukuza uchumi wa eneo husika’’. Aliongeza Waziri Lukuvi.
Waziri huyo wa ardhi ameongeza kuwa Benki nyingi Mkoani Shinyanga zina fedha nyingi ambazo hazina wakopaji kutokana na watu wa Shinyanga kukosa dahamana ya inayowezesha kukopa akionya kuwa kuna baadahi ya Wilaya hazifanya mipango yoyote ya uendelezaji ardhi kwa kipindi cha miaka mitano mpaka sasa.
Kufuatia hali hiyo Wizara yake imeanzisha kila Mkoa Ofisi ya Ardhi yenye vifaa pamoja na wataalamu watakaosaidia Mkoa kutatua changamoto za Ardhi zilipo na ofisi hizo zitakuwa na mtaalam wa kila Sekta ya Ardhi na ni Ofisi za Wizara ya Ardhi zitakazo kuwa zinafanya kazi kila mkoa kwa lengo la kuweka huduma karibu na wananchi.
Waziri Lukuvi ameonya kuwa kuanzia sasa wananchi hawatakuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata hati katika makao makuu ya mkoa badala yake ni Afisa Ardhi atakayekuwa akienda katika ofisi za Wilaya husika kutoa hati kwa wananchi chini ya usimamizi wa Afisa Ardhi wa Wilaya husika akiongeza kuwa hii itaongeza mwitikio wa wananchi kupima ardhi yao.
Pamoja na masuala mengine Waziri Lukuvi amewataka vingozi katika ngazi ya Wilaya kupima ardhi ya vijiji ambavyo tayari vina umeme na vimeanza kuwa na tabia za miji kupima maeneo hayo mapema ili vitakapoanza kuwa miji viwe tayari vina ardhi iliyopimwa kwa maendeleo ya baadae ya mipangao miji