Home Mchanganyiko Mweli akoshwa na matumizi ya tofali za mfungamano katika ujenzi wa madarasa

Mweli akoshwa na matumizi ya tofali za mfungamano katika ujenzi wa madarasa

0

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), toka OR-TAMISEMI Gerald Mweli (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel wakati wa ziara yake ya kikazi
mkoani humo.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), toka OR-TAMISEMI (kwanza kulia) akimskiliza Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel (katikati) akielezea ujenzi wa madarasa
kwa kutumia tofali mfungamano wakati wa ziara yake mkoani humo, kushoto ni
Katibu Tawala Mkoa wa Geita Denis Bandisa.

Muoenekano wa darasa lililojengwa kwa kutumia tofali mfungamano katika shule ya sekondari Nyanza iliyopo Geita Mji, Darasa hilo limegharimu shilingi milioni 11
tu.

Naibu Katibu Mkuu(E),OR-TAMISEMI (mbele katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel (kulia), Mkurugenzi wa usimamizi wa Elimu OR-
TAMISEMI Julius Nestory (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa kikao cha waratibu wa Elimu Kata, Wakuu wa shule pamoja na walimu wakuu wa Geita.

Mkurugenzi wa usimamizi wa Elimu OR-TAMISEMI Julius Nestory (Kulia) akizungumza na Waratibu wa Elimu Kata, Wakuu wa shule pamoja na walimu wakuu wa Geita wakati wa kikao nao kilichofanyika kwenye shule ya Sekondari
ya wasichana ya Nyankumbu.

Baadhi ya Waratibu wa Elimu Kata, Wakuu wa shule pamoja na walimu wakuu wa Geita wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Naibu Katibu Mkuu(E) OR- TAMISEMI na kufanyuka kwenye shule ya Sekondari ya wasichana ya
Nyankumbu.

******************************

Nteghenjwa Hosseah, Geita.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Gerald Mweli amefurahishwa na ubunifu wa kutumia tofali mfungamano (Interlock) kwenye ujenzi wa
vyumba vya madarasa katika kubaliana na mlundikano wa wanafunzi katika shule za Mkoa wa Geita.

 

Mweli ameonyesha furaha yake wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo iliyokua na lengo la kukagua miundombinu ya Elimu iliyojengwa na inayoendelea kujengwa pamoja
na kupokea changamoto za walimu na kuzitolea ufafanuzi.

 

Akiwa Mkoani Geita Mweli aliweza kujionea namna ambavyo Mkoa huo umejiongeza kwa kupeleka mashine za kufyatulia matofali mfungamano katika Halmashauri zote na kujenga darasa la mfano kwa kutumia tofali hizo katika shule ya sekondari nyanza.

 

Akikagua darasa hilo Mweli amesema ubunifu ni wa kuigwa na Mikoa mingine sababu umeonyesha umakini wa hali ya juu wa viongozi wa Mkoa wa Geita, uzalendo, kujitoa na kupunguza changamoto ya uhaba wavyumba vya madarasa katika shule za Serikali.

 

“Nimefarijika sana kuona darasa limekamilika kwa kutumia matofali haya ambayo ni ya gharama nafuu kwani sasa gharama za ujenzi wa chumba cha darasa kwa mkoa wa Geita imeshuka kutoka shilingi milioni 20 mpaka kufikia milioni 11 tu hili ni jambo zuri na la mfano nawapogeza sana Geita” alisema Mweli.

 

Mweli aliongeza kuwa Geita ni miongoni mwa mikoa yenye uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa na shule zake nyingi zina wanafunzi wengi mno kiasi kwamba hata
ufundishaji wa wanafunzi hao inakuwa changamoto lakini viongozi wa mkoa huu wamejiongeza na kuja na ubunifu huu wa kupunguza gharama za ujenzi kwa kutumia
matofali mfungamano na kwa mpango huu tutaweza kujenga vyumba vingi zaidi na kupunguza changamoto ya mlundikano wa wanafunzi.

 

Akizungumzia mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel amesema wao kama viongozi hawataki mpaka waagize kutoka juu wanabainisha changamoto
walizonazo, wanaweka mikakati mapema, na kuanza kutekeleza kwa wakati na kutatuza changamoto zao.

 

“Mahitajia ya vyumba madarsa katika Mkoa wetu ni zadi ya vyumba 9000 na tunategemea wanafunzi wengine watamaliza shule hivi karibuni hivyo mahitaji yataongezeka zaidi ya sasa tunajiandaa mapema kukabiliana na mahitaji tuliyonayo”
alisema Mhe. Robert Gabriel.

 

 

Aliongeza kuwa mashine hizi za kufyatulia matofali ya mfungamano zilikuwepo tangu zamani lakini hazikuwa zikitumika, nikaona ni muda sasa kuzigawa kwa kila
halmashauri kuwaelekeza namna ya kuzitumia ili nao waanze kufyatua matofali ya kujengea madarasa: Kwa hapa Geita tumeshajenga darasa moja la mfano katika shule ya Sekondari Nyanza kwa kutumia tofali hizi na tumelikamilisha kabisa kwa kutumia gharama ya shilingi Mil 11 tu hivyo watu wote nawakaribisha waje hapa wajionee darasa hili.

 

Naye Mkurugenzi wa usimamizi wa Elimu OR-TAMISEMI Julius Nestory wakati wa kikao na waratibu wa elimu Kata, wakuu wa shule pamoja na walimu wakuu aliwakumbusha wataalamu hao kuwa sifa za kuwa kiongozi wa Elimu ni lazima uwe na uwezo wa kuwasimamia walio chini yako, kufanya maamuzi na kuyasimamia na kuhakikisha kuwa unaishi karibu na eneo lako la kazi.

 

Mkurugenzi Nestory aliwakumbusha Waratibu wa Elimu kata kuwa ni lazima wawe na barua za utezi wa nafasi hiyo, wawe na shahada husika na wakae kwenye kata
aliyopangiwa na si vinginevyo.

 

Naibu Katibu Mkuu Mweli akiwa katika Mkoa wa Geita alitembelea shule ya sekondari nyanza, kalangalala shule ya msingi pamoja na shule ya mchepuo wa Kingereza ya
bombambili.