Kikao cha kujadili tishio la ugonjwa wa corona baina ya Serikali na shirika la afya duniani, Mabalozi na wakuu wa taasisi za kimataifa na wadau wa sekta ya afya kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya afya jijini Dar es salaam
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa (UN) Zlatan Milisic akichangia kwenye mkutano huo
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kutoka mashirika na taasisi wakifuatilia mkutano huo
Waziri Ummy Mwalimu akiongea kwenye kikao kilichojadili kwa pamoja tishio la mlipuko wa ugonjwa wa corona
Mkurugenzi wa idara ya dharura na maafa kutoka wizara ya afya Dkt. Elias Kwesi akiwasilisha mada kwenye kikao cha kujadili kukabiliana na Corona
Katibu Mkuu wizara ya afya Dkt. Zainab Chaula akiongea kwenye kikao hicho
Mratibu wa dharura na maafa kutoka WHO akiwasilisha mada
………………………………………………..
Na. Catherine Sungura-Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya na wadau wa sekta ya afya ikiwa na lengo la kujadili kwa pamoja tishio la mlipuko wa ugonjwa wa corona.
Waziri Ummy amesema kikao hicho waliwaeleza wadau kama taarifa ya shirika la afya duniani(WHO) ilivyotangaza hali ya maambukizi ya ugonjwa huo duniani hivyo kama serikali ni vyema kuwapatia taarifa wadau hao
“Tumewapa taarifa wadau wetu na kuwahakikishia kwamba tanzania hakuna mtu mwenye maambukizi mwenye maambukizi ya virusi wa corona na tumewaeleza hatua gani kama serikali tumezichukua katika kujiandaa kukabiliana na tishio hili”.
Katika kikao hicho waziri ameeleza kwamba wizara yake imeweza kuchukua hatua ya kukabiliana na tishio hilo kwa kuimarisha ufuatiliaji katika maeneo mbali mbali ikiwemo kwenye viwanda vya ndege na viingilio vingine ikiwemo bandarini.
Hata hivyo Waziri Ummy amesema kwamba wameweza kutoa mafunzo kwa baadhi ya wataalamu wa afya waliopo mikoani pamoja na kuandaa dawa, vifaa na vifaa tiba endapo nchi itapata mshukiwa wa virusi vya corana.
“Tumewaomba washirikiane nasi katika kuhakikisha kwamba sasa tunakua tayari kukabiliana na tishio hilo hata kama hatuna mgonjwa hii tulikuabaliana kwenye mkutano wa nchi wanachama wa SADC kwamba nchi zote tunaingia kwenye hatua ya kukabiliana”.Alieleza Waziri Ummy.
Katika kikao hicho amesema kuwa wamewaomba wadau waunge mkono katika kutoa mafunzo zaidi hususan kwa wataamu wote wa afya ili kuwakinga na maambukizi pamoja na kutoa elimu na taarifa sahihi kwa wananchi nchini.
Wadau hao wameishukuru serikali kupitia wizara ya afya kwa kuwashirikisha na wameridhika kwa hatua zilizochukuliwa katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huo.Kikao hicho kiliwashirikisha shirika la afya duniani(WHO),Mabalozi na Wakuu wa taasisi za kimataifa hapa nchini.