Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Zungu akieleza mikakati ya ofisi yake katika kuvutia wawekezaji wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020.
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali katika Kongamano hilo.
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020.
**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wananchi wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya biashara kwani serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha fursa zinapatikana kwaajili ya wananchi wake.
Ameyasema hayo leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki na Wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Uswidi na Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano Serena Hotel Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Machi, 2020.
Akizungumza katika Kongamano hilo Waziri Kairuki amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa Korona kongamano hilo limeweza kupatikana kwa makampuni takribani 20 toka nchini Sweden na vilevile zimeweza kuja kampu i kutoka nchini Burundi,Rwanda,Kenya na nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo wananchi wanatakiwa kutumia fursa kama hizi ili kuweza kuleta maendeleo ya kiuchumi.
“Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu tumeendelea kuzijengea uwezo Benki zetu za Kibiashara, za Kilimo, Benki zetu za Uwekezaji pamoja na nyinginezo na hata hivyo ,Ofisi ya Waziri Mkuu NSSF,AZANIA,SIDO,VETA pamoja na Baraza la Wananchi Kiuchumi wameanzisha mfuko mwingine maalumu utakaosaidia watu ambao watahitaji kuanzisha viwanda vya kati na viwanda vya juu na kupitia mfuko huo utakuwa na viwango vya aina mbili, kiwango cha kwanza kitakuwa mikopo ya Milioni 8 mpaka Milioni 50, kiwango cha pili kitakuwa mikopo kuanzia Milioni 50 mpaka Milioni 500, kupitia mikopo hiyo hakuna kuweka dhamana”. Amesema Waziri Kairuki.
Aidha Waziri Kairuki amesema kuwa wengi walikuwa wanalalamikia kuhusu biashara na uwekezaji lakini ndani ya uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano ilipo chini ya Rais Mhe.Dkt.John Magufuli mengi ymefanyika kwani hakuna kodi yoyote ambayo ameianzisha au mawaziri wake kupitia sekta mbalimbali kuanzishwa.
“Ndani ya Uongozi huu Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ameweza kukubali kufutwa kwa kodi,tozo zaidi ya 168 ndani ya miaka miwili ukiangalia katika sekta ya Kilimo pekee kulikuwa na tozo 146 lakini ndani ya mwaka mmoja tozo za sekta ya kilimo pekee zimeweza kufutwa 105”. Amesema Waziri Kairuki.
Pamoja na hayo ametoa rai kwa Wananchi waweze kujitokeza katika kongamano la Uwekezaji linaloendelea katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam ili kuweza kujitengenezea fursa za kibiashara kupitia kongamano hilo kwani kuna kampuni takribani 20 kutoka nje ya nchi zimeshiriki.
Nae Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe.Mussa Zungu amewataka wale wote ambao wamekuwa wakisumbuliwa katika masuala ya vibari vya mazingira wamfuate ili awese kuwapatia vibari hivyo pasipokuwa na usumbufu wa aina yoyote.