Ofisi hizo Magomeni jijini Dar kuhusu Mkutano
wao mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei 9 mwaka huu na kwamba Kitapitisha Mgombea wa
Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.
Chama cha Tanzania Labour Party (TLP,Richard Lymo akizungumza jambo
mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo kwenye makao Makuu ya
Ofisi hizo Magomeni jijini Dar kuhusu Mkutano
wao mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei 9 mwaka huu na kwamba Kitapitisha Mgombea wa
Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli. Pichana Michuzi JR-Michuzi Media.
Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kuwa Mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika Mei 9 mwaka huu uttampitisha Mgombea wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao mkuu ya chama hicho Magomeni Usalama jijini Dare es salaam Mwenyekiti wa Chama hicho Agustino Latonga Mrema amesema kuwa jina la Mgombea Urais limepitishwa na Halmashauri Kuu Chama na kilichobaki ni kudhibitisha jina la Mgombea huyo.
Amesema kuwa katika uchaguzi mkuu hakuna haja ya kuweka Mgombea wa Urais kutokana na Rais aliyepo kwa sababu amekidhi mahitaji ya watanzania kwa asilimia mia moja.
“Hivi unasimamishaje Mgombea wakati Kazi aliyoifanya Rais aliyepo madarakani inaonekana, kungekuwepo na tatizo ndio kungekuwepo na ulazima wa kusimamisha mgombea mwingine “amesema Mrema
Aidha Mrema amemshauri Mwenyekiti wa chama Cha NCCR Mageuzi James Mbatia kuutangazia umma kuwa Uchaguzi Mkuu utakuwa wa Uhuru na Haki pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais aliyepo madarakani.
Amesema Mbatia alishawahi kusema kuwa kusifu serikali iliyopo madarakani sio dhambi hivyo anaweza kuendelea kuunga mkono Rais wa Awamu ya Tano kuendelea kwa kipindi kingine.
Mrema amesema Rais Dkt.John Magufuli aachwe amalize malengo yake kuifikisha Tanzania anayoitaka ambayo ni Tanzania ya Maendeleo yanayoonekana.
Amesema TLP si chama cha kufuata upepo wa bendera bali ni chama kinachojua kinachofanyika na kuukubali uongozi wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Amesema vyama vingine vijifunze na kuangalia Rais Dkt.John Magufuli namna Tanzania ilivyopata Maendeleo kwa kipindi kifupi ikiwamo kukomesha Rushwa.