Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Kasimu Majaliwa akiwa katika makaburi ya wahanga wa Ajari ya Moto iliyotekea Agost 10 Mwaka jana eneo la Msavu Mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Kasimu Majaliwa Akiwa na vingozi wa dini katika eneo la makaburi ya wahanga wa Ajari ya Moto iliyotekea Agost 10 Mwaka jana eneo la Msavu Mkoani Morogoro.
Muonekano wa nje katika eneo la Makaburi ya kola Manispaa ya Morogoro,ambapo pia wamezikwa wahanga wa ajari ya moto.
**************************
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasimu Majaliwa Amefanya ziara katika makaburi ya wahanga wa Ajari ya Moto iliyotekea Agost 10 Mwaka jana, yaliyoko katika eneo la kola Manispaa ya Morogoro, katika kujiridhisha na maagizo aliyoyatoa ya kujengwa Uzio katika Makaburi hayo.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa ameridhishwa na kazi za awali ziliozanzwa kutekelezwa na uongozi wa Mkoa huo ,ikiwa ni pamoja na kupokea ombi la kujengwa Mnara katika makuburi hayo , huku akiwataka Baadhi ya viongozi kutekeleza majukumu yao ili kufikia lengo lililowekwa na Serikali .
Hata hivyo amegiza kila Mwaka kuwe na kumbukumbu ya kuwaenzi Wahanga hao,huku akitaka kujengwa kwa eneo maalumu ambalo litatumika kama sehemu ya kufanyia ibada kwa ndugu na jamaaa watakaofika katika eneo hilo kwa lengo la kuwafanyia dua ndugu zao.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema kuwa hadi sasa ujenzi wa Uzio wa makaburi hayo umetumia zaidi ya milloni 10 , huku miili liyozikwa katika eneo hilo ni 76 , kati ya hao 50 wawetambulika na ndugu zao.
Ikumbukwe kuwa Agost 10,2019 katika eneo la Msavu Manipaa ya Morogoro lori la mafuta lilipinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta na kusababisha vifo vya watu mia moja kumi tano(115) kati ya hao wanaume 109 na wanawake 6.