Home Mchanganyiko MBOWE NA VIONGOZI WENZAKE WA CHADEMA WAHUKUMIWA KULIPA MILIONI 350 AMA KWENDA...

MBOWE NA VIONGOZI WENZAKE WA CHADEMA WAHUKUMIWA KULIPA MILIONI 350 AMA KWENDA JELA

0

**********************

Leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu viongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kulipa faini ya jumla ya shilingi milioni 350 au kifungo cha miezi mitano kwa kila kosa baada ya kuwakuta na hatia ya mashtaka 12.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi mkuu, Thomas Simba ambaye amesema upande wa mashtaka umethibitisha makosa yao bila kuacha shaka yoyote katika makosa yote 12 isipokua shtaka la kwanza la kupanga kufanya mkusanyiko usio halali kwa sababu mahakama haijaweza kuthibitisha kosa hilo.