Home Michezo CORONA YASIMAMISHA LIGI KUU YA ITALIA KWA MUDA

CORONA YASIMAMISHA LIGI KUU YA ITALIA KWA MUDA

0

MICHEZO yote ndani ya nchi ya Italia imesimamishwa kwa muda kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini Italia ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu ya Serie A na Tokyo Olympics.

Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte amethibitisha hayo Machi 9, Jana Jumatatu kwenye Television.

Conte amesema :”Kuna tatizo kubwa kwa sasa ni lazima tuangalie namna ya kupambana nalo leo kwa ajili ya kesho.

” Kwa wale wakazi wanaotaka kusafiri kwa usalama wa afya yao ni lazima wawe na sababu maalumu zitakazowafanya waweze kuondoka ndani ya Italia.

¬†“Kwetu sisi ninaona afya na kukua kwa watu wetu ni bora na lazima tufanye jambo bora kwa ajili ya watu wetu,” amesema.

Juventus ni vinara wa kuchukua taji la Seria A wakiwa wametwaa mara 35 na kwenye ligi pia ni vinara wakiwa na pointi 63 wakiwa wamecheza mechi 26.