MICHEZO yote ndani ya nchi ya Italia imesimamishwa kwa muda kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini Italia ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu ya Serie A na Tokyo Olympics.
Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte amethibitisha hayo Machi 9, Jana Jumatatu kwenye Television.
Conte amesema :”Kuna tatizo kubwa kwa sasa ni lazima tuangalie namna ya kupambana nalo leo kwa ajili ya kesho.
” Kwa wale wakazi wanaotaka kusafiri kwa usalama wa afya yao ni lazima wawe na sababu maalumu zitakazowafanya waweze kuondoka ndani ya Italia.
“Kwetu sisi ninaona afya na kukua kwa watu wetu ni bora na lazima tufanye jambo bora kwa ajili ya watu wetu,” amesema.
Juventus ni vinara wa kuchukua taji la Seria A wakiwa wametwaa mara 35 na kwenye ligi pia ni vinara wakiwa na pointi 63 wakiwa wamecheza mechi 26.