Jumla ya watazamaji 59,325 wameweza kuingia na kuangalia mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kati ya Yanga na Simba katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mapato ya mchezo huo ni Milioni 545.4 (545, 422,000) kwa tiketi za VIPA, B &C , machungwa na Mzunguko.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limetoa taarifa ya mapato ya mchezo namba 270 kati ya Yanga na Simba uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa timu hizo mbili, ulizikutanisha timu hizo na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 goli lililofungwa na Benard Morrison.
Mechi hiyo iliyoweka historia ya kwanza nchini, imeweza kutazamwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Ahmad Ahmad na Rais wa TFF Walace Karia.
Mbali na hao viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwamo Waziri mwenye dhamana na michezo Dkt Harrison Mwakyembe, watendaji wa BMT, Mawaziri, Wabunge, Wasanii na watu mashuhuri walihudhuria pia.