*******************************
Nteghenjwa Hosseah, Shinyanga
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Elimu OR-TAMISEMI Gerald Mweli amehoji kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa Mkoa wa Shinyanga Kitaifa kutoka nafasi ya 3 kwa mwaka 2018 hadi nafasi ya 13 kwa mwaka 2019.
Akizungumza katika ziara yake ya kikazi Mkoani humo amesema haiwezekani kwa kipindi cha mwaka mmoja Mkoa huo kuporomoka kitaaluma kwa kiwango hicho jambo lililomfanya aanzie ziara yake Mkoani hapo ili kufahamu kulikoni na namna walivyojipanga kurudi katika nafasi nzuri zaidi kitaifa.
“Akielezea sababu za kuporomoka huko Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Afisa Elimu Mkoa huo Mohamed Kahundi amesema tatizo kubwa lililopo ni uhaba wa walimu haswa wa masomo ya Sayansi, uchakavu wa miundombinu pamoa na hulka ya Mkoa huu wa kupendelea ufugaji hivyo kuhamasisha watoto kwenda kufuga kuliko kuzingatia masomo.
“Tunajitahidi sana katika kuhakikisha tunatoa elimu bora lakini upungufu wa walimu haswa katika masomo ya Sayansi umechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma jitihada wa kupandisha kiwango cha elimu katika Mkoa huu” alisema Kahundi.
Aidha Kahundi aliongeza kuwa uchakavu wa miundombuni katika baadhi ya shule piani miongoni mwa changamoto zinazoshusha ari ya walimu kufundisha kwa ufanisi lakini pia na wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumzia hulka ya kupenda kuchunga kuliko masomo amesema wazazi wa Mkoa huu haswa ameneo ya pembezoni hupendelea kuwapeleka watoto machungani lakini sio kumshawishi mtoto kutumia muda wake wa mapumziko kujisomea hivi vyote kwa ujumla vimechangia katika kushusha kiwango chetu cha Elimu kwa kipindi husika alisisitiza Kahundi.
Naibu Katibu Mkuu Mweli amesema haoni kama sababu zilizoainishwa zinaweza kuchangia moja kwa moja kushusha kiwango cha Elimu kwa sababu changamoto hizo sio ngeni katika mazingira yao na ilikuwaje katika mwaka 2018 kufanya vizuri na mwaka uliofutia kufanya kushuka je ni kwamba changamoto hizo zimetokea baada ya mwaka huo au zilikuwepo kwa kipindi chote.
“Nimezipoeka lakini hazijanishawishi na inabidi kushughulikia kila moja kwa namna yake kama ni ya miundombinu ishughulikiwe kimiundombinu na kama ni ya Kitaalumu halkadhalika nayo iweze kushughulikiwa kitaaluma” alisema Mweli.
Kwa sasa hivi tunarekebisha miundombinu katika shule nyingi Nchini kupitia mradi wa Lipa kulingana na matokeo(Paying for Result – Ep4r), shule nyingi sana Nchini tumeshazifikia na kupitia ziara hii pia tumekuja kuona uchakavu wa shule za Mkoa huu ila nazo ziweze kufanyiwa marekebisho hivyo hili sasa litakwisha na sitarajii kuliskia tena kama changamoto alisisiza.
Aliongeza kuwa changamoto iliyoibaini kutokana na taarifa hiyo ni usimamizi; Nina mashaka na usimamizi kuanzia kwenye Waratibu wa Elimu Kata, Walimu Wakuu, Walimu wa Taaluma pamoja na walimu katika kufundisha vipindi ipasavyo.
Suala la upungufu wa walimu sioni kama ni changamoto katika Mkoa huu maana walimu wa masomo ya sanaa takwimu zinaonyesha wapo wa kutosha je hawa wanafanya kazi ipasavyo kabla hamjaanza kuomba hao walimu wa Sayansi tunataka kuona hawa waliopo wamefanya kazi kwa kiasi gani na imeleta matokeo chanya kwa kiwango gani alihoji Mweli.
Hivyo tuongeze nguvu katika ksuimamia katika ngazi ili kila mtu atimizie wajibu wake nina uhakika mtarudi kwenye kiwango kile au hata na zaidi kwa sababu tayari mlionyesha mnaweza na nitapenda kuona mafanikio yale ya mwaka 2018 yanafikiwa.
Naibu Katibu Mweli katika ziara yake Mkoani Shinyanga mefanya kikao na wasimamizi wa Elimu sambamba na kutembelea shule ya ufundi Mwadui , shule mpya ya wasichana inayoendelea kujengwa hapo hapo Mwadui zote zipo katika Halmashauri ya Kishapu kuangalia uchakavu wa miundombinu na namna Serikali inavyoweza kuchukua hatua za makusudi za ukarabati ili kuboresha utoaji wa Elimu.
Kupitia ziara hiyo pia Mweli atatembelea Mkoa wa Geita, Mwanza pamoja na Simiyu.