……………………………………………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim
Wanawake kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wameungana na wanawake wengine Duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika leo katika Shule ya Msingi Mkonze Jijini Dodoma.
Katika maadhimisho hayo wanawake wametakiwa kujitokeza katika kugombea nafasi za uongozi katika kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020.
Wito huo umetolewa leo na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Felister Bura wakati wa maadhimisho ya wanawake duniani ambapo kimkoa yamefanyika Shule ya Msingi Mkonze Jijini Dodoma, na kitaifa mkoani Simiyu.
“Mwanamke ukijitokeza kugombea wanamke wenzako tutakupa ushirikiano ili kuhakikisha unafikia malengo yako ya kulitumikia taifa ili katika nafasi utakayo gombea”, ameeleza Bi. Bura
Akizungumza Bi. Bura amewataka wakina mama kuwa mawakili wa jamii ili kubadili fikra zao katika kuhakikisha mtoto wakike na mwanamke wanapata haki zao kwa ufasaha.
Lakini pia Bi. Bura ameongezea kuwa wakina mama mnajukumu la kusimamia maendeleo yam toto wakike katika kupata elimu ili aweze kutimiza ndoto zake kwani bila hivyo Watoto wetu wakike wanakutana na changamoto nyingi mpaka wanashindwa kufikia malengo yao.
“Mwanamke sio mtu wa kunyanyaswa kwani naye anahaki ya kupata mahitaji na kuishi kwa amani kama mwanaume, hivyo nivyema wanaume mkatambua thamani ya wanawake kwa kuwashirikisha na kuwapa usikivu katika mipango ya maendeleo ya familia,” amesema Bi.Bura
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Dodoma Mjini Mwalimu Fatuma Hassani amewataka wakinamama kupaza sauti kwa mamlaka husika ili kuhakikisha wanapinga unyanyasaji wakijinsia ili wakina mama washiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa taifa .
Ikumbukwe Kila mwaka tarehe 8 Machi wanawake duniani kote huadhimisha siku ya wanawake duniani, ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Simiyu na kwa hapa Jijini Dodoma yamefanyika Shule ya Msingi Mkonze.