Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi Mshindi wa Shaba Christina Charles katika halfa ya kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo
Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi Mshindi wa pili wa Fedha Amina Hamisi katika halfa ya kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo
Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu ya wanawake ya Lugalo katika halfa ya kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo
Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Watoto waliopata Zawadi katika halfa ya kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo
Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji mbalimbali mara baada ya kufunga mashindano ya kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani kwa Mchezo wa Gofu yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
……………………………………………………………………………………………………..
Na Luteni Selemani Semunyu
Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete amewataka wanawake nchi kusimama imara katika kujiendeleza katika nyanja mbali mbali ikiwemo michezo na kuliletea Taifa heshima bila kujali tofauti za jinsi walizonazo.
Aliyasema hayo wakati akifunga Mashindano ya kuadhimisha siku ya mwanamke duniani kwa mchezo wa Gofu katika yaliyofanyika Jana katika Uwanja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Mama Salama alisema licha ya michezo mingi kuonekana kuchezwa na wanaume na wanawake kuingia katika michezo hiyo sasa ni wakati kwa wanaume kucheza michezo iliyokuwa ainaonekana kama ya wanawake kama mpira wa pete.
” Kama tatizo ni Mavazi basi zitafutwa nguo za aina Nyingine zitakazotumika katika mchezo huo ili kuhakikisha wanashiriki wanaume kama ambavyo wanawake wanashiriki. “ Alisema Mama Salma Kikwete.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema anajivunia mafanikio makubwa ya Klabu ya Lugalo kwa mafanikio makubwa yaliyoletwa na wanawake kutokana na kuleta Vikombe ndani na Nje .
“ Kiukweli tangu nimekuwa Mwenyekiti wa Lugalo sijawahi kupata kikombe kutoka kwa wanaume hasa ya Nje ya Nchi lakini Wanawake wamekuwa wakinitoa kimasomaso na najivunia na imekuwa changamoto kwa Wanaume katika kufanya Vizuri, Alisema Mwenyekiti Lugalo.
Kwa upande wake Nahodha wa Wanawake wa Lugalo Hawa Wanyenche alimuomba Mama Salma kuwa Mlezi wa Timu ya Wanawake na kuweza kusaidia ikiwemo Timu ya Taifa ya Wanawake.
Kwa upande wa Matokeo ya Mashindano hayo Mchezaji Angel Eaton alifanikiwa kuibuka Mshindi wa Jumla baada ya kupata Mikwaju 80 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni Tatu huku katika Fedha Mshindi ni Salma Juma akifuatiwa na Amina Hamisi.
Wakati katika Shaba Mshindi ni Christina Charles aliyepata Net ya 74 huku katika kundi la Wanawake wenye umri Mkubwa Ladies Senior Mshindi ni Stephani Sayore.