Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga yaliyofanyika leo Ijumaa Machi 6,2020 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo yakiongozwa na Kauli ya “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akiwasihi wanafunzi kuzingatia masomo yao kwa kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zao ikiwemo kupata mimba za utotoni.
Wanafunzi na wazazi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Kishapu.
Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilaya ya Kishapu vinavyosimamiwa na TGNP, Peter Nestory akisoma taarifa fupi kuhusu vituo 9 vya taarifa na maarifa wilayani Kishapu. Aliipongeza Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa kutenga bajeti ya taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi pamoja juhudi kubwa ya kuunda na kutoa elimu kwa kamati za MTAKUWWA.
Meza kuu wakimsikiliza Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wilaya ya Kishapu vinavyosimamiwa na TGNP, Peter Nestory wakati akisoma taarifa fupi kuhusu vituo 9 vya taarifa na maarifa wilayani Kishapu.
Mwanaharakati wa haki za wanawake, Fredina Saidi ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa wanawake akipigania ajenda za wanawake tangu mwaka 2003 akiwahamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Wanafunzi na wadau wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Josephat Swalala akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Kishapu.
Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Kishapu.
Afisa Mradi asasi ya Relief to Development Society (REDESO),Elica Karutha akielezea namna wanavyotekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake na vijana wilayani Kishapu ili waweze kujikwamua kiuchumi leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba (kushoto) akicheza muziki na wadau wa haki za wanawake kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba (katikati) akicheza muziki na wadau wa haki za wanawake kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Wanawake/wadau wa haki za wanawake wakicheza muziki wakati nyimbo zinahusu masuala ya wanawake zipigwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Kishapu.
Wanawake/wadau wa haki za wanawake wakicheza muziki wakati nyimbo zinahusu masuala ya wanawake zipigwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Kishapu.
Wanawake/wadau wa haki za wanawake wakicheza muziki wakati nyimbo zinahusu masuala ya wanawake zipigwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Kishapu.
Wanawake wakicheza muziki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Wanawake wakicheza muziki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo.
Wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yanaendelea kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi wakicheza muziki.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Machi 6,2020 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba.
Maadhimisho hayo yakiongozwa na Kauli ya “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa nay a baadae”,yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwigumbi,kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo na kuhudhuriwa na wadau wa haki za wanawake ukiwemo Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) unaotekeleza kazi zake wilayani Kishapu.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo,Talaba aliwakumbusha wanawake kuwa wao ni watu jasiri,siyo waoga hivyo wana kila sababu ya kufanya mambo makubwa kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
“Wanawake ni jeshi kubwa,wanawake ni jasiri,wenye upendo kwelikweli,ni walimu katika familia. Msiwe wanyonge na kusubiri kuwezeshwa. Leo nawapa Kanuni moja ya maisha ambayo ni ‘ Ukitaka kufanikiwa weka alama ya kutoa kwenye mambo yanayokukwamisha na weka alama ya kujumlisha kwenye mambo mazuri”,alisema Talaba.
“Ukikaa mahali kwa kutegemea kuhurumiwa na wanaume utakuwa unajikwamisha mwenyewe. Ongeza juhudi na maarifa katika kazi unazofanya kwani wanawake tunaweza na tuna nafasi kubwa kuleta mabadiliko katika jamii. Kuolewa siyo kikwaza cha wewe kusonga mbele,mkumbuke kuwa siku hizi wanaume wanapenda kuoa wanawake wenye kazi.Hivyo fanyeni kazi kwa bidii kwani ukiwa na kipato chako hakuna mwanaume atakayefanyia ukatili”,alisema.
Aidha aliwataka wanawake kupunguza chuki kwa wanawake wenzao wanaothubutu kugombea nafasi za uongozi.
“Kuna watu wanasema wanawake hatupendani,mimi nawataka wanawake tupunguze chuki na tuongeze upendo”,alisema Talaba.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuikumbusha jamii umuhimu wa kusomesha watoto wa kike akibainisha kuwa elimu ndiyo inatengeneza mfumo wa maisha ya baadaye.
“Naomba ndugu zangu tupeleke shule watoto wote wa kiume na wa kike. Tuwalinde watoto wetu ili wamalize shule,tusiwaozeshe wangali wadogo.Ukisomesha mtoto hautabaki kama ulivyo.
Nanyi watoto wa kike fungeni vibwebwe mkatae mimba,mmalize masomo yenu ili mtimize ndoto zenu”,alisema Talaba.
Kwa upande wake Katibu wa Vituo vya Taarifa na Maarifa 9 wilaya ya Kishapu vinavyosimamiwa na TGNP, Peter Nestory aliishukuru Serikali ya Tanzania kuendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kimataifa kupinga ukatili wa aina zote ikiwemo uwakilishi sawa katika vyombo vya maamuzi na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
“Uwakilishi katika vyombo vya maamuzi kama vile katika serikali za vijiji au mitaa, Udiwani,Ubunge na Mabaraza mbalimbali yanasaidia kumuwezesha mwanamke kupaza sauti ili kufikia Mpango wa Hamsini kwa Hamsini baina ya wanawake na wanaume”,alisema Nestory.
“Ili kufikia malengo ya 50% kwa 50% katika vyombo vya uwakilishi ni lazima wanawake wajitokeze kwenda kugombea nyadhifa mbalimbali kwani bado idadi ya viongozi wanawake ni ndogo. Mikakati madhubuti inahitajika ili kufikia mikakati hii ya 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030”,aliongeza Nestory.
Aidha aliipongeza Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kwa kutenga bajeti ya taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi pamoja juhudi kubwa ya kuunda na kutoa elimu kwa kamati za MTAKUWWA.
Alisema Mtandao wa Jinsia (TGNP) umekuwa ukiendesha uhamasishaji na uelimishaji ili kuboresha utendaji wa viongozi na wanawake ambapo hatua hiyo ya TGNP ni ya kujivunia na kupongezwa kwa kila mwanamke.
Naye Mwanaharakati wa haki za wanawake, Fredina Saidi ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa wanawake akipigania ajenda za wanawake tangu mwaka 2003 aliwataka wanawake wanaogombea nafasi za uongozi kutokata tamaa.
“Kama una nia ya kuwa kiongozi simama imara,usitetereke wala kujali kauli zinazovunja moyo ikiwemo ya ‘mwanamke akiwa kiongozi atashindikana,atakuwa Malaya,atatawala mwanaume’.Kuwa jasiri na amini unaweza kuwa kiongozi”,alisema Saidi.