Home Mchanganyiko Mlemavu mwenye ndoto ya kusimama kwa ‘miguu yake’

Mlemavu mwenye ndoto ya kusimama kwa ‘miguu yake’

0

**************************

NA MWANDISHI WETU

KILA binaadam katika dunia hii ana matatizo yake ya kimaisha, hali ambayo inasababisha kila mmoja kusaka namna ya kufikia malengo kupitia kwa wadau mbalimbali ambao ndio kimbilio la ufanikishwaji huo.

Kwa mazingira ya sasa, wadau wanaweza kutoa msaada kwa jamii ama mdau mmoja mmoja kwa mujibu wa hitaji la mhusika.

Boniface Mokami (25), mlemavu wa miguu ambaye ni mmoja wa mfano  wa wadau wenye uhitaji wa kuwezeshwa kwa usafiri aweze kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato halali katika kujikwamua na umasikini.

Katika mahojiano na Tanzania Daima, Mokami anasema licha ya kuzaliwa akiwa na hali hiyo a ulemavu, amaanini akisaidiwa kupata usafiri, ataweza kujishughulisha na kazi mbalimbali za kujitafutia kipato kwa ajili ya kujikimu.

Mokami anasema, sababu hasa ya kuamua kufikisha ujumbe wake kwa jamii, ni kupata msaada wa kitendea kazi kimwezeshe kushiriki kazi za kujipatia kipato cha kuendesha maisha na kuacha kuwa ombaomba.

Hivyo, kilio chake kwa jamii ni kusaidiwa Bajaj itakayosaidia kufanikisha kipato chake kupitia chombo hicho, kwani ndio kimbilio lake la kwanza ingawa ana fani nyingine alizozipata katika masomo yake.

Kwa kuanzia, kuelekea kupatiwa msaada huo wa Bajaj, ameomba kibali maalum kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ili kufanikisha lengo lake hilo asiangukie katika kundi la vijana ambao wamekuwa wakishiriki utapeli. 

“Kwa kuwa nahitaji nisaidiwe Bajaj ambayo gharama yake ni kubwa, nimeanzia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo ili iwe njia rahisi ya kufikia malengo ninayo yahitaji,” anasema Mokami na kuongeza:

“Nilijaribu kuomba msaada kwa kuchangisha fedha nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kupata bajaj, nikaona ni bora sualamlangu nilifikishe serikalini ili niweze kufanikiwa,” anasema.

Mokami anayeishi maeneo ya Changanyikeni, karibu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa wazazi wa rafiki yake Noel ambaye ni mlemavu pia, walifahamiana tangu wakiwa shule wakati huo.

“Ni muda mrefu niko kwa wazazi wa rafiki yangu Noel, kwa kuwa muda unazidi kwenda naona ni bora nijiongeze kusaka namna ya kujitegemea na kusaidia wenzangu.

“Kwa haraka, haraka uendeshaji wa Bajaj kibiashara utakuwa ni msaada mkubwa kwangu,” alisema Mokami na kuongeza

“Fursa ya kuendesha Bajaj ndio kimbilio la haraka ambalo linaweza kunisaidia katika maisha yangu, hata kutembea kwangu ni kwa shida, itanisaidia kufanya safari zangu na hapo hapo nitafanikisha kipato change,” anasema Mokami.

Mokami ambaye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa familia ya Noel Mokami wa Tarime, mkoani Mara  ambaye hupata shida ya kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana na ulemavu alionao, fani nyingine aliyo nayo ni Graphics Design akiwa na elimu ya msingi aliyosoma mwaka 2016.

Kabla ya kusomea Graphics, alipata elimu ya sekondari katika shule ya Moshi Tech kuanzia mwaka 2000, ingawa alishindwa kuendelea na elimu ya juu baada ya kukosa sifa ya kufika huko.

Baada ya kumaliza Moshi Tech. alirudi nyumbani Tarime, japo katika miaka minne aliyokuwa masomoni hakuwahi kurejea nyumbani kwa  ukosefu wa fedha ambazo zingefanikisha kufika nyumbani kwao.

Mokami anasema aliishi mkoani Kilimanjaro kwa njia ya kusaidiwa na wadau kwani wazazi hawakuwa na uwezo kifedha.

Kwa upande wa fani ya Graphics, anasema ameisomea jijini Dar es Salaam akitokea Changanyike hadi Kimara Temboni alikokuwa akifuata elimu hiyo ya Graphics akisema moja ya changamoto ni sehemu ya kutekeleza majukumu yake, inahitajika duka mbalo atauza vifaa vya ofisi na shuleni.

Mokami anasema, hivi sasa wakati akijipanga kwa ajili ya kusubiri Bajaj hiyo, anajaribu kupita kwa baadhi ya rafiki zake kuomba msaada huo ili afikie malengo yake.

“Msaada ninaopata kwa sasa kutoka kwa baadhi ya wadau ni mdogo, hauwezi kufanikisha ununuzi wa Bajaj, nawaomba wadau hapa nchini wanisaidie ili nifanikishe hatua ninayoifikiria,” anasema Mokami.

Anaweka bayana kwamba alianza darasa la kwanza mwaka 2001-2008, elimu aliyoipata Jeshi la Wokovu Kurasini nafasi aliyoipata kutoka kwa baba yake mlezi, Francis Machela ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya awali wilayani Tarime.

Machela ndiye alifanikisha Mokami kujiunga na jeshi la Wokovu na kupata elimu ambako akiwa shuleni alicheza Mpira wa Meza, mchezo ambao uko ndani ya damu yake ingawa kwa sasa anafikiria Bajaj kwanza.

Mbali ya ushabiki wake wa mpira wa meza, pia ni shabiki wa muziki wa miondoko ya RnB  na kueleza kwamba ana mapenzi makubwa na mwanamuziki Young D.

Mokami ni mtoto wa kwanza katika familia yao ya watoto wanne, wadogo zake wanamtegemea kwa masuala mbalimbali ikiwemo elimu.

Mokami anapatikana kwa namba 0763273650/0652572448