Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Skooine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akiwa ameshikilia moja ya vitabu hivyo baada ya kukabidhiwa, Kulia kwake ni Naibu makamu mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Prof. Peter Gillar, kuanzia kshoto ni Mkurugenzi wa Maktaba ya taifa ya Kilimo Prof. Mugyabuso Lwehabura, Bwana Derek Murusuri ambaye ndiye mwandishi wa kitabu na Dkt. Cliford Tandali aliyetoa msaada huo wa vitabu
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akifurahi jambo na Dkt. Cliford Tandali wakati akisoma kitabu hicho kabla ya kupokea vitabu hivyo.
Viongozi hao wakizungumza kabla ya kuanza rasmi zoezi la kukabidhi na kupokea vitabu.
Ukurusa wa Mbele wa kitabu hicho unavyoonekana na kusomeka.
Dkt. Cliford Tandali wa pili kushoto akieleza lengo la kutoa msaada huo vitabu kwa SUA , kulia kwake ni Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda.
*****************************
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amewashauri wanataaluma na Watanzania wengine kuona umuhimu wa kuyaandikia vitabu mawazo yao mbalimbali ambayo yatasaidia kubadili fikra na mitazamo ili kuchochea maendeleo ya Tanzania.
Wito huo ameutoa wakati akipokea Vitabu kumi vyenye thamani ya shilingi laki nne vilivyotolewa na Mwanafunzi wa SUA ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Cliford Tandali kitabu kilichoandikwa na bwana Derek Murusuri kinachoitwa Making Africa world’s largets Economy yaani Kuifanya afrika kuwa yenye uchumi mkubwa Duniani.
Prof. Chibunda alisema kuna watu wengi wenye mawazo mazuri ambayo yanaweza kuisaidia Tanzania na afrika lakini wamebaki nayo kichwani mwao na wengine wanaandika na kuishia njiani na hivyo kuifanya jamii na taifa kushindwa kunufaika na mawazo yao mazuri.
“Nakupongeza sana bwana Derek kwa kufanikiwa kuandika na kukamilisha kitabu hiki ambacho kinakwenda sasa kwa jamii kukisoma ili kuleta maendeleo ya taifa letu na Afrika kwa ujumla,na mawazo yako yataishi hata utakapoondoka duniani’’ Alisisitiza Prof. Chibunda.
Kwa upande wake Dkt. Cliford Tandali amabye ndiye aliyetoa Msaada wa vitabu hivyo kumi kwaajili ya Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA alisema kuwa wanafunzi wa somo taaluma za maendeleo na ndaki ya Sayansi za jamii na insia kitawafaa sana kutokana na mawazo mazuri yaliyowekwa kwenye kitabu hicho.
Dkt. Tandali alibainisha kuwa kitabu hicho baada yay eye kukisoma kinaonyesha kwa uwazi na undani namna ambavyo nchi mbalimbali duniani zimefanya na kupiga hatua kimaendeleo hasa katika matumizi ya sayansi na teknoloji na sasa wako mbali hata wale ambao tulipata uhuru pamoja nao.
“Mabara mengine yamesonga mbele kwa kuzingatia sayansi teknolojia na ubunifu hivyo sisi kama watanzania tuna kila sababu ya kuikumbatia Sayansi teknolojia na ubunifu ili tuweze kupiga hatua kwa haraka kama ambavyo wenzetu wamefanya’’Alisisitiza Dkt. Tandali.
Aliongeza kwa kusema kuwa SUA ndio mahali ambapo masomo ya sayansi yanafundishwa na teknolojia zinazalishwa hivyo nitoe wito kwa Serikali kuona sababu ya kutenga fungu maalumu ili matokeo ya tafiti hizo ziweze kusambazwa na kuisaidia jamii ya Watanzania hasa zile za kilimo,mifugo na uvuvi.
Nae kwa upande wake Mwandishi wa kitabu hicho kilichozinduliwa na Waziri Mkuu Mstafu Mhe. Mizengo Pinda amemshukuru Katibu Tawala wa Mstaafu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Cliford Tandali kwa kutimiza maagizo ya Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda aliyoitoa wakati akizindua kitabu hicho ya kutaka kitabu hicho kisambazwe vyuo vikuu ili vijana wengi Zaidi wakisome.
Akielezea malengo ya kuandika kitabu hicho alisema ni kuwaamsha,kuwatia chachu vijana wa Afrika kuwa wanaweza kulifanya bara la Afrika kuweza kushindana kiuchumi nan chi za mabara mengine kwa kubadili mitazamo,kuchapa kazi na kutumia maliasili zilizopo.
‘’Hili linawezekana kabisa kwa kuvunja kizuizi cha utamaduni kuwa hatuwezi hasa kwa vijana wetu walio kwenye vyuo vikuu na taasisi zingine katika kutumia teknolojia na ubunifu kama njia muhimu ya kuleta mageuzi katika eneo hilo nyeti na muhimu katika karne ya sasa inayotegemea sana sayansi na teknolojia’’ Alisisitiza Derek Murusuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Mugyabuso Lwehabura akipokea vitabu hivyo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo ameahidi kuvitunza na kuwapatia wanafunzi na watumiaji wa Maktaba hiyo kuvisoma na uhitaji ukiwa mkubwa wataongeza idadi yake ili mawazo ya mwandishi wa kitabu yatimie.