********************
TBS yawahimiza wanafunzi wa shule za Sekondari Mpanda na Rungwa zilizopo Manispaa ya Mpanda kuzingatia ununuzi wa bidhaa zenye ubora ili kuepuka hasara na athari za kiafya. Vilevile walikumbushwa kusoma taarifa mbalimbali zinazopatikana kwenye vifungashio za bidhaa kama vile muda wa kuisha matumizi. Wanafunzi hao walishukuru TBS na kuahidi kuwa mabalozi wa masuala ya ubora. Jumla ya wanafunzi 2116 walipata elimu hiyo.