……………………………………………………………………………………….
Na Farida Saidy,Morogoro
Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Muunano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa ameeleza kusikitishwa na kitendo cha wakala wa Barabara Nchini (TANROAD) kushindwa kurejesha mawasiliano ya barabara ya Morogoro – Dodoma kwa siku tatu sasa, huku akisema kitendo hicho ni uzembe na kulizalilisha taifa ukizingatia Barabara hiyo ni Kiungo kati ya Tanzania na Mataifa mbalimbali.
Mpaka Leo March 4,2020 Ni siku ya tatu sasa tangu kukosekana kwa mawasiliano ya barabara katika eneo hilo la Kiyegeya, na hii ni baada ya Daraja la mto Mkange kusombwa na maji,ambapo kwa Sasa abiria pekee ndio wakilazimika kuvuka upande wa pili kwa miguu kutafuta usafiri mbadala baada ya Magari makubwa ya Abiria nay ale ya mizigo kushindwa kupita.
Toka Jumatatu March 2, majira ya saa 10 jioni iliporipotiwa Daraja hilo kusomwa na Maji,huku jitihada mbalimbali zimefanyika kurejesha mawasiliano,Na viongozi mbalimbali wakilazimika kukesha eneo la tukio lakin inaonekana Hali kuwa bado si swari.
Hata hivyo Waziri mkuu Kassim Majaliwa amefika kujionea hali halisi katika eneo Hilo ambapo amesema kitendo Cha TANROAD kushindwa kurejesha Barabara hiyo ni uzembe wa Hali ya juu.
Aidha amemtaka waziri mwenye dhamana ya ujenzi,Uchukuzi na mawasiliano, kuongeza usimamizi kwa kuomba nguvu ya ziada toka jeshi la wananchi pamoja na Timu ya wataalam wa Ujenzi kutoka Mikoa ya Morogoro na Dodoma.
Waathirika wakubwa ni Madereva wa Mabasi na Magari mengine ya Mizigo, wanaasema pamoja na kuahidiwa Daraja hilo lingekamilika mapema hadi sasa wanaendelea kuishi kwa shida ukizingatia eneo lenyewe hakuna huduma za kijamii.
Pamoja na mambo mengine waziri mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ujenzi huo kufanyika usiku na mchana kuwezesha ndani ya saa 24 mawasiliano yanarejee kuwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea.