*********************
Bodi ya ligi ya shirikisho la soka nchini Tanzania imetangaza mwamuzi Martin Saanya kutoka Mkoani Morogoro kuwa ndiye mwamuzi atakayepuliza kipyenga katinga mchezo wa watani wanjadi Kati ya wenyeji Yanga Dhidi ya Simba jumapili ya March 08-2020 uwanja wa Taifa jijini Daresalaam.
Katika mchezo huo Saanya atasaidia wa mwamuzi Namba Moja (Line One) Mohamed Mkono Kutoka Tanga, Mwamuzi Namba Mbili (Line Two) Frank Komba wa Daresalaam, Na Mwamuzi wa Mezani (Fourth Official) Elly Sasii wa Daresalaam.
Lakini katika kile kinachoonekana Ni kupunguza Malalamiko juu ya waamuzi na kuhakikisha mchezo huo unachezeshwa kwa ubora TPLB imetangaza waamuzi wawili wa ziada ambao watasimama kwenye mstari wa goli kwa lugha ya kimpira wanatambuliwa Kama Goal Line Refferees ambao Ni Abdallah Mwinyimkuu wa Singida Na Ramadhani Kayoko wa Daresalaam.
Mtathimini was waamuzi katika mechi hiyo atakuwa Ni Sudi Abdi wa Arusha na Kamishina wa mchezo Ni Mohamed Mkweche wa Daresalaam.
Mara ya kwanza na ya mwisho Tanzania Kutumia muundo huu was waamuzi ilikuwa Ni mwaka 2019 wakati wa mechi za hatua ya robo Fainali ya Michuano ya Afcon U17 iliyofanyika jijini Daresalaam.
Mchezo huu wa jumapili unatarajiwa kuhudhuliwa na Rais wa CAF Ahmad Ahmad ambaye pia atakuwa Ni mgeni wa Heshima siku hiyo ya mechi