Home Mchanganyiko KIKAO KAZI CHA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI CHAAHIRISHWA

KIKAO KAZI CHA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI CHAAHIRISHWA

0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi anawataarifu  Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini pamoja na wadau wengine kuwa Kikao Kazi kilichotarajiwa kufanyika tarehe 9 hadi 13 Machi 2020, Jijini Mbeya kimeahirishwa.

Kikao kazi hicho hufanyika kila mwaka ili kuwajengea uwezo Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali namna ya kutangaza shughuli za Serikali na kuhakikisha,  Idara na Vitengo vya Mawasiliano na Uhusiano Serikalini vinaimarishwa ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano na Teknolojia mpya ya Habari na Mawasiliano katika kuwahudumia wananchi.

Aidha, Maafisa hao wametakiwa kuendelea  kutekeleza majukumu yao katika maeneo ya kazi kwa kutangaza utekelezaji wa Serikali ili wananchi waweze kupata taarifa muhimu za Serikali. 

Imetolewa na:-

Lorietha Laurence

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.