Home Biashara UWEKEZAJI MINADA YA DHAMANA ZA SERIKALI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 103

UWEKEZAJI MINADA YA DHAMANA ZA SERIKALI WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 103

0

Meneja wa Usimamizi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Lameck Kakulu akiwasilisha mada ya mwitikio wa wawekezaji kuwekeza kwenye dhamana za Serikali katika semina ya waandishi wa habari inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha.

Bw. Victor Tarimu Meneja Usimamizi wa Benki za Huduma Ndogo za Fedha na Maduka ya Kubadilishia Fedha za Kigeni akiwasilisha mada katika semina hiyo inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha.

Mwanasheria wa Benki Kuu ya Tanzania Amedeus Shayo akiwasilisha mada kuhusu sheria ya Huduma ndogo za fedha katika semina hiyo.

Msemaji wa Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja akichangia mada katika semina hiyo.

Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na watoa mada.

Dk. Deogratias Assey Meneja Udhibiti wa Ustahimilivu wa Sekta ya Fedha na Usimamizi wa Majanga akiwasilisha mada kuhusu udhibiti na ustahimilivu wa fedha.

Bw Richard Malisa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana Benki Kuu ya Tanzania BoT akiwasilisha mada kuhusu kazi za bodi hiyo.

Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki akimkaribisha Meneja wa Usimamizi wa Usimamizi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Lameck Kakulu ili kutoa mada katika semina hiyo.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango wa pili kutoka kulia na Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki  wa kwanza kulia pamoja na maofisa wa BoT tawi la Arusha wakifuatilia majadiliano katika semina hiyo.

……………………………………………………

Meneja wa Usimamizi wa Usimamizi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Lameck Kakulu amesema kwa kipindi cha mwaka  kuanzia juni mpaka Desemba 2019 Benki Kuu imeshuhudia kuongezeka kwa uwekezaji kwenye minada ya  dhamana za serikali.

Amesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 103 ukilinganisha na kiwango ambacho serikali ilipanga kukikopa katika kipindi hiki cha nusu ya mwaka.

Bw. Lameck Kakulu ameongeza kuwa hii imeeenda sambamba na kupungua kwa riba hasa za dhamana za serikali ambapo zimepungua kutoka asilimia 8.5 mpaka 5 kwa kipindi kama hicho mwaka 2018/19.

Bw. Lameck Nakulu amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasilisha mada ya  mwitikio wa wawekezaji kuwekeza kwenye dhamana za Serikali katika semina ya waandishi wa habari inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha.

Ameongeza kuwa kwa upande wa washiriki mabenki yameendelea  kuongezeka kwenye kushiriki kutoka asilimia 67 huku mifuko ya Pensheni ushiriki wao katika minada ukipanda kutoka asilimia 8 mpaka asiimia 20 na kwa upande wa wekezaji binafsi mwitikio umepanda kutoka asilimia 2 mpaka 6 hata ambapo hivyo uko chini BoT ingependa uongezeke zaidi.

“Ongezeko hili linatokana na jitihada za Benki Kuu na Wizara ya fedha kufanya uhamasishaji na na kuwapa uelewa wadau wa shughuli za kiuchumi kwamba ukiwekeza kwenye dhamana za serikali huwezi kupoteza fedha zako ulizowekeza”.

Kipato ni kikubwa kwa sababu riba zinazotolewa  kwenye hizi dhamana za seikali ni kubwa na unao uwezo wa kuziuza kwenye soko la upili na pia unaweza kuzitumia kama dhamana katika taasisi zingine za fedha ili kukopa”. Amesema Bw. Lameck Nakulu.

Ameongeza kuwa ili kuongeza ushiriki wa wawekezaji wadogo BoT imeendelea na jitihada kwa kushirikiana na CMSA na Wizara ya Fedha kuhakikisha kwamba inaendeleza Platfom ambayo itasaidia wawekezaji wadogo kushiriki kikamilifu katika minada ya dhamana za serikali ambayo inaweza kukamilika kukamilika mwakani.

Wawekezaji wadogo wataweza kushiriki kwenye minada kwa kutumia simu na kwa kiwango kidogo cha fedha, kwa sababu kiwango cha sasa cha shilingi 500 bado kinonekana ni kikubwa na tunadhani hilo litaongeza kwa kiasi kikubwa wawekezaji wadogo kushiriki katika shughuli za uchumi wa nchi na kuongeza pato la serikali.