Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika utafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 5, Machi 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni “Kukuza Soko la Ajira na Mahusiano Mema Sehemu za Kazi kwa Maendeleo Endelevu”