Kaimu Meneja wa Kampuni ya Ranchi zaTaifa Bw.Masele Shilagi akiwa ofisi ya meneja wa ranchi ya Kongwa,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa zoezi la uchanjaji mifugo katika ranchi za NARCO zote zinazonguka ranchi ya Kongwa,jijini Dodoma.
Afisa Mifugo Msaidizi Mwandamizi Idara ya uzalishaji na Masoko kutoka wizara ya mifugo na Uvuvi Bw.Charles Lugamara,akizungumzia mikakati ya wizara hiyo katika uzalishaji wa mifuko.
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Ranchi zaTaifa Bw.Masele Shilagi mwenye tai akizungumza na Mwenyekiti wa Umoja wa wafugaji waliokodishwa vitalu 28 vya Ranchi ya Kongwa Bw.Ngonyani Uledi,alipowasili kwenye eneo la liliandaliwa kuchanja mifugo ya wafugaji katika kijiji cha Maucha wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma.
Baadhi ya wafugaji wakiwa kwenye eneo la liliandaliwa kwa ajili ya kuchanja mifugoi katika kijiji cha Maucha wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma.
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Ranchi za Taifa Bw.Masele Shilagi akichanja ng’ombe wa Umoja wa wafugaji waliokodishwa vitalu vya ranchi katika kijiji cha Maucha,kilichopo wilaya ya Kongwa ,jijini Dodoma kama ishara ya uzinduzi wa zoezi la uchanjaji mifugo katika Ranchi zote nchini.
Baadhi ya ng’ombe walioletwa na wafugaji kwa ajili ya kupata chanjo kijiji cha Maucha waliokodishwa vitalu 28 katika ranchi ya Kongwa.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Jumla ya ng’ombe 24,999 katika vitalu vya Ranchi ya Kongwa mkoani Dodoma wamepatiwa chanjo kwa ajili ya kukabiliana na homa ya mapafu na mapele ngozi.
Hayo yameelezwa jana na Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa(NARCO), Masele Mipawa, katika zoezi la utoaji chanjo ya mifugo kwa wafugaji wanaozunguka Ranchi hiyo.
Amesema Ranchi ya Kongwa ina ukubwa wa hekta 38,000 ambapo hekta 12076.6 limetengwa vitalu kwa ajili ya wafugaji wanaozunguka ranchi hiyo.
Amesema katika kutekeleza mpango wa uthibiti wa magonjwa na kuwa eneo huru, Ranchi hiyo ilianza kuchanja mifugo ya wananchi kulingana na kalenda ya chanjo.
“Tumeanza zoezi hili Februari 21, mwaka huu kwa ng’ombe ambapo wanapatiwa chanjo ya homa ya mapele ngozi, mapafu na magonjwa mengine tupo hatua za mwisho kukamilisha zoezi, na mwitikio ni mzuri,”amesema.
Kwa upande wake, Ofisa Mifugo Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Charles Lugamara, amesema ulaji wa mazao ya mifugo kwa watanzania ni hafifu ambapo kwasasa mtu mzima anakula nyama kilo 15 kwa mwaka.
Amesema Kwa mujibu wa kiwango kilichowekwa na Shirika la Chakula Duniani, mtu mmoja anatakiwa kula kilo 50 za nyama kwa mwaka.
Amebainisha ulaji wa nyama bado upo chini licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi zaidi ya Milioni 32.
“Licha ya kuwa na mifugo mingi, tija ya mazao ya mifugo bado ni ndogo, ndio maana wizara ina mikakati mingi ya kuboresha sekta ya mifugo ili mazao yanayozalishwa yawe ni bora,”amesema.
Ametaja miongoni mwa mikakati ambayo ipo mbioni kutekelezwa ni uzalishaji nyama kwa ajili ya soko la nje ambao unalenga kutatua kero zinazowakabili wazalishaji ili kuzalisha nyama bora kukidhi mahitaji ya ndani na nje.
Ofisa huyo amesema kupitia NARCO, wizara imejipanga wafugaji waliopewa vitalu watazingatia misingi ya uzalishaji kwa kuzalisha nyama itakayokidhi ubora na uchanjaji mifugo.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa wafugaji waliokodishwa vitalu 28 vya Ranchi ya Kongwa Bw.Ngonyani Uledi,amesema kuwa wanatarajia kuchanja mifugo yote iliyopo ndani ya ranchi hiyo na ile ambayo iko jirani lengo kubwa ni kudhibiti magonjwa hatari ya mifugo.
Bw.Masele ametoa rai kwa wananchi waliokodishwa vitalu vya kufugia kuhakikisha wanachanja mifugo yao na wafugaji watakao kaidi watachukuliwa hatua kali za kisheria.