Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na
washiriki wa Bonanza la kuibua vipaji vya uimbaji lililofanyika mwishoni mwa wiki wilayani
Same mkoa wa Kilimanjaro lililoongozwa na kaulimbiu “Tutambue vipaji vyetu tujiajiri kufikia
uchumi wa kati na JPM.”
Baadhi ya washiriki wa Bonanza la kuibua vipaji vya uimbaji lililofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro lililoongozwa na kaulimbiu “Tutambue vipaji vyetu tujiajiri kufikia uchumi wa kati na JPM.”
Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Senyamule akitoa taarifa fupi juu ya tamasha la kuibua vipavi vya uimbaji wilayani humo kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuongea na hadhira iliyohudhuria bonanza hilo kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa sanaa kwa vijana na ajira ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa banda la mjasiriamali bibi Enighenja Mbwambo akionesha na kuuza baadhi ya bidhaa za kiutamaduni wakati wa Bonanza la kuibua vipaji vya uimbaji lililofanyika mwishoni mwa wiki wilayani
Same mkoa wa Kilimanjaro lililoongozwa na kaulimbiu “Tutambue vipaji vyetu tujiajiri kufikia uchumi wa kati na JPM.”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akimkabidhi maiki mwanafunzi Jamila Jafari (wa kwanza kulia) aliyefanikiwa kuimba wimbo wa mwanamuziki Elias Barnabas (Barnaba Boy, wa katikati) wa “Namtaka wife material ninayefanana naye”wakati wa Bonanza la kuibua vipaji vya uimbaji wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Same)