Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Salum Manyata,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya utoaji dawa za usingizi salama wakati wa upasuaji kwa kina mama wajawazito yanayofanyika jijini Mbeya kwa siku tatu kwa kushirikisha wataalamu kutoka vituo vya afya na hospitali zilizoko Nyanda Juu kusini.
Dkt Shuwaikha Mkufunzi wa mafunzo akitoa maelekezo jinsi ya kumudumia mgonjwa wakati wa kutoa dawa ya usingizi kabla ya upasuaji
Sehemu ya wataalam washiriki wa mafunzo elekezi ya utoaji dawa ya usingizi salama wakati wa ufungizi wa mafunzo hayo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Salum Manyata akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wawezeshaji wa mafunzo elekezi ya utoaji dawa za usingizi salama wakati wa upasuaji kwa kina mama wajawazito kutoka ndani na nje ya nchi katika ukumbi wa Usingilo jijini Mbeya
……………………………………………………………………………………………………
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Salum Manyata amesema wataalamu wa kutoa dawa za usingizi nchini wana wajibu wa kuboresha utoaji wa huduma kwa kina mama wajawazito na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa upasuaji.
Dk. Manyata ameyasema leo wakati akifungua mafunzo elekezi ya utoaji dawa za usingizi salama wakati wa upasuaji kwa kina mama wajawazito yanayofanyika jijini Mbeya kwa siku tatu na kushirikisha wataalamu kutoka vituo vya afya na hospitali zilizoko Nyanda Juu kusini.
Amesema kuwa ni vema washiriki hao kutumia fursa walioipata ya mafunzo hayo ili kutekeleza yale ambayo wameyapata kwa kutoa huduma salama na sahihi.
Dk. Manyata amewaasa wataalamu hao kupeleka mrejesho wa masuala mbalimbali mapya waliyoyapata kwa wengine katika vituo vyao watakaporejea ili kuhakikisha taratibu zote zinasimamiwa vizuri.
Amebainisha lengo ni kupunguza vifo vya kina mama wajawazito wakati wote wa upasuaji.
Mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi kutoka ndani na nje ya nchi na kushirikisha wataalam 35 wa dawa za usingizi kutoka Nyanda za Juu Kusini na kufadhiliwa na Chama cha Madaktari Bingwa wa dawa za usingizi duniani (WFSA) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa dawa za usingiizi Tanzania (SAFE).