Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya ujenzi Ziana Mlawa (Katikati)akiwataka wanawake kuchangamukia fursa za ujenzi wa matengenezo ya barabara wakati wa kufungua mafunzo ya siku 12 yaliyofanyika mkoani Morogoro ambayo ni mafunzo ya hatua za awali za ukandarasi kwa kutumia teknolojia stahiki na nguvu kazi .
Washiriki hao wa mafunzo ya wanawake katika kutekeleza ukandarasi kwa kutumia teknolojia na nguvu kazi yaliyofanyika chuo cha ujenzi mkoani Morogoro wakitazama na kufatilia kwa makini ushauri wa Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya ujenzi Ziana Mlawa.
Mratibu wa kitengo cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara mhandisi Gradness Kitaly akitoa taarifa ya mafuzo kwa mgeni rasmi Ziana Mlawa na changamoto zinazowakabili wanawake katika kujisajiri ili kutekeleza shughuli za ujenzi na matengenezo ya barabara .
Wanawake kutoka mikoa nane hapa nchini waliohudhuria mafunzo ya ukandarasi kwa kutumia teknolojia stahiki na nguvu kazi mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Ziana Mlawa (watatu kutoka kulia ) akifatiwa na mkuu wa chuo cha ujenzi Mkoani Morogoro Mlyapali.
Wanawake waliohudhuria mafunzo ya ya awali ya ukandarasi kwa kutumia teknolojia stahiki na nguvu kazi yaliyofanyika mkoani Morogoro wakifatilia kwa makini maelekezo ya mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wizara ya ujenzi Ziana Mlawa (hayupo kweye picha).