***********************
Timu za soka za chini ya miaka 13, 15 na 18 za shule ya Msingi Atlas Madale msingi na sekondari zimeingia fainali.
Timu hizo zinefuzu kuingia fainali katika kombe la Afrisoccer linalochezwa katika viwanja vya shule ya kimataifa ya Laureate iliyopo Mbezi Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi mkuu wa michezo wa shule ya Atlas, Solomon Ondego aliniambia blogu hii kuwa katika mechi tatu za chini ya miaka 13 timu ya Atlas ilitoka kidedea kwa kuzifunga timu za Afrisoccer na St. Mary’s mabao matatu kwa sifuri huku ikitoka sare ya moja kwa moja na Shamsiye.
Katika mechi za chini ya miaka 15 wababe wa Atlas walitoka sare ya moja kwa moja na timu ya Afrisoccer huku wakizibugiza mabao matatu kwa sifuri timu za shule za St Mary’s na Academic.
Katika mechi za walio chino ya miaka 1i. Atlas ilitoka sare ya bao mona kwa moja na timu za Academic na Afrisoccer huku ikiibugiza mabao mawili bila timu ya Shamsiye.
Fainali ya mashindano ya Afrisoccer yaliyoanza ha a zinachezwa leo katika viwanja hivyo vya Laureate mbezi beach.
Vinara waliofunga mabao ya Atlas katika mechi chini ya miaka 13 ni
ROBERT MUIGU na
ISAIH EZEKIEL .
*UNDER katika mechi ya chini ya miaka kumi na tano
HEMEDI BUYOYA
ANTONY ALPHONCE na
MUHAMED MUSA.
Waliotikis nyavu chini ya miaka 18 ni
HAMISI SALUM,
HANCE MUGAMBI na
HAMISI SALUM