Mshambuliaji wa Aston Villa,Mbwana Samatta ameandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga bao kwenye Fainali ya League Cup maarufu kama ”Carabao” mchezo uliopigwa uwanja wa Wembley.
Mbwana Samatta akiifungia Aston Villa bao la kufutia machozi ikichapwa 2-1 na Manchester City katika fainali ya Kombe la Ligi England leo Uwanja wa Wembley PICHA ZAID GONGA HAPA
Samatta amefunga bao dakika ya 41 akiunganisha kwa kichwa cha kupiga mbizi baada ya kupokea pasi toka kwa Anwar El- Ghazi.
Kufunga kwa bao hilo linamfanya Samatta kuwa Mchezaji wa tano kutoka Bara la Afrika kufunga kwenye Fainali ya League Cup wengine ni Didier Drogba (4), Joseph-Désiré Job, Obafemi Martins na Yaya Touré ambao kila moja amefunga bao moja.
Man City walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa mshambuliaji wao Sergio Aguero dakika ya 20 na kiungo Rodri kufunga la pili dakika 34.
Kwa ushindi huo unaifanya Man City kufanikiwa kututea ubingwa wake baada ya kuifunga Aston Villa 2-1 mchezo ambao ulikuwa na upinzani mkali kwa kila timu kushambuliana kwa zamu.