Kutoka kulia anayetoa maelezo ni Dkt Chitopela Mganga Mkuu, Samwel Bundala Mhandisi wa Wilaya, Hudson Kamoga Mkurugenzi Mtendaji, Michael Faraay Afisa Mipango, Respitius Kagaruki Mweka Hazina, Juma Mvumo Afisa Manunuzi na Isaya Sisya Mkaguzi wa Ndani.
****************************
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbilu Mhe.Hudson Kamoga akiwa na timu ya wataalam wa Halmashauri wametembelea kujionea ujenzi wa hospitali ya Wilaya hiyo na kufurahishwa na hatua ilipofikia.
Akizungumza katika hospitali hiyo Mhe.Kimoga amesema kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ni moja ya hatua kubwa za uboreshaji wa sekta ya afya unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John Pombe Magufuli.
Amesema kuwa Serikali inayojali maisha ya watu, inawaza pia na kujali afya zao.
HAta hivyo Hospitali hiyo itakapoanza kutoa huduma itawanufaisha zaidi ya wakazi 220,000 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu waliokuwa wakitegemea Hospitali ya Rufaa ya Haydom pekee.
Ujenzi huo umegharimu Shilingi Bilioni 1.5 fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.