Home Mchanganyiko MAMLAKA YA UDHIBITI NA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI YATOA ELIMU KWA...

MAMLAKA YA UDHIBITI NA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI [TIRA] YATOA ELIMU KWA WAANDISHI WA HABARI UMUHIMU WA BIMA KATIKA JAMII

0

Mkurugenzi wa kuendeleza soko la bima na utafiti ,mamlaka ya
Usimamizi wa bima Tanzania,Bi,Adelande  Muganyizi,akiwasilisha mada mbalimbali kwa waandishi wa habari wa Dodoma wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu umuhimu wa bima kwa jamii.

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa bima[TIRA]kanda ya kati Stella Rutaguza,akizungumza wakati wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo  waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa bima kwa jamii.

Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia maada mbalimbali kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo  waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa bima kwa jamii.

Mwaandishi wa habari Mwandamizi kutoka Gazeti la Mwananchi Habel Chindawale akiuliza swali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo  waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa bima kwa jamii.

……………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa bima nchini [TIRA]imetoa Mafunzo
ya kuwajengea uwezo Wanahabari umuhimu wa bima katika jamii  kwani ni
moja ya suluhisho kwa Majanga  .

Akiwasilisha mada mbalimbali katika Mafunzo hayo jijini
Dodoma,Mkurugenzi wa kuendeleza soko la bima na utafiti ,mamlaka ya
Usimamizi wa bima Tanzania,Bi,Adelande  Muganyizi amesema bima
husaidia kupunguza maumivu ya majanga mbalimbali ikiwa  ni pamoja na
majanga ya moto,ajali,ukame,na mafuriko hivyo wanahabari wanatakiwa
kuwa mabalozi wazuri  katika kuelimisha jamii umuhimu wa bima kwani
huondoa umasikini.
“Majanga hayabigi hodi lakini bima inasaidia kupunguza sana maumivu
yaliyotokana na majanga ,hivyo  tunatakiwa tuelewe sana haki ya
usalama katika mali zetu pindi tunapokumbwa na majanga kwa hiyo
tunapoongelea suala la bima ni usalama wa afya,Usalama wa mali
zetu”amesema.
Aidha,Bi.Muganyizi ameanisha kanuni za msingi za  mkataba wa bima ni
pamoja na kuwepo na uhusiano unaotambulika kisheria[Insurable
interest],uaminifu wa hali ya juu[ultmost  faith], kumrejeshea mkata
bima thamani halisi kabla ya janga kutokea pamoja na kuchangia hasara
endapo mali moja imechangiwa na makampuni ya bima zaidi ya moja.

Akizungumzia kuhusu bima ya lazima,Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa
bima[TIRA]kanda ya kati Stella Rutaguza amesema kwenye magari ya
usafiri wa umma kila abiria aliyebebwa anatakiwa awe amekatiwa bima.

“Tukija kwenye suala hili naona kama kuna changamoto kidogo ,lakini
kuhusu bima ya lazima inatakiwa kila abiria aliyebebwa kwenye gari la
usafiri wa umma awe amekatiwa bima na mwenye jukumu hilo ni mmiliki wa
gari husika,kama gari lako lina uwezo wa kibeba abiria 55 na sheria
inataka hivyo hivyo ukate bima ya watu wa idadi kama hiyo”amesema .
Pia,Rutaguza amesema moja ya kanuni kubwa  ya bima ni kuwa hairuhusiwi
kuikatia bima mali isiyokuwa ya kwako hata kama ni ya ndugu  huku
akitaja aina mbalimbali za bima zikiwa ni pamoja na bima za
kilimo,bima za ndoa,bima za dhima za umma ,bima za makosa ya kitaaluma
,bima za wizi ,bima za waajiriwa  ,bima za maisha,bima za elimu  na
bima za vifo.
Meneja usimamizi wa Maendeleo ya Masoko ,Kutoka Mamlaka ya Usimamizi
na udhibiti wa bima Tanzania[TIRA]Bw.Edgar Shao amesema TIRA ina
jukumu la kusajili kampuni za bima pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.